HACHIKO THE DOG.
Huyu alikua ni mbwa aliyezaliwa November 10 mwaka 1923 katika Shamba moja Huko japan. Mbwa Huyu alikua akimilikiwa na Profesa mmoja aliyekua akifundisha chuo cha Tokyo Imperial University .
Mbwa Huyu alilelewa na bwana huyo aliyejulikana kwa jina la Hidesaburo Ueno na mara kwa mara alikua akimsindikiza Profesa huyu kwenda chuoni huko na kumsubir katika kituo kimoja cha treni na Ilikua ni kawaida kufanya hivyo kumsubir na kurud nae nyumbani.
Mnamo 21 may ya mwaka 1925 bwana Ueno alipokwenda chuoni hakurud tena nyumban na mbwa huyo aliendelea kumsubir hapo bila kuchoka .Watu walianza kuvutiwa na mbwa huyo mtiifu kwakua walishawahi kumuona mara kadhaa akiwa na profesa kituoni hapo inasemekana mbwa huyo alikaa miaka tisa akisubirii bwana Ueno afike kituoni Hapo , Watu walikua wana mtunza mbwa huyo sehem hio na kumpatia chakula kipindi chote alichokua akisubiri.
Hachiko alikufa march 8 mwaka 1935 akiwa na umri wa miaka 11 chanzo kikiwa ni kansa na minyoo.
Unaweza Kutafuta Movie Inaitwa A DOG'S TALE ukachekii kisa chake.
No comments:
Post a Comment