UHUNI WA WEST COAST NA EAST COAST ULIVYOTOA FURSA KWENYE "DO FOR LOVE" YA 2PAC

UHUNI WA WEST COAST NA EAST COAST ULIVYOTOA FURSA KWENYE "DO FOR LOVE" YA 2PAC
.
.
Mambo yaliyoendelea kwenye muziki wa hip hop miaka ya 90 yalibadilisha upepo kabisa kutoka kuwa muziki wa harakati na kuwa muziki uliosheheni matendo ya kihuni na uhalifu.Kundi la NWA likiongozwa na Dr Dre na Ice Cube  walienda mbali zaidi pale walipoingia studio na kurekodi wimbo wa kuridhalilisha jeshi la polisi ulioitwa "f**k the police".

Mauaji ya Big L,2pac Shakur,Yaki Kadafi,Notorious Big,kujihusisha na biashara na matumizi ya dawa za kulevya hakuna mzazi aliyejisikia fahari tena kuona mwanae anafanya muziki huo.

Ilifikia hatua wafuasi wa ngome za pwani ya magharibi (West Coast) na pwani ya mashariki (East Coast) kwenda kambi pinzani kuchukuliana wasichana warembo.Vuta nikuvute zilizoendelea kati ya ngome hizi mbili hasimu za West Coast na East Coast zilipelekea kuwapoteza  magwiji wa muziki huo 2pac Shakur aliyeuwawa mwaka 1996 na Notorious Big mwaka 1997.

Miaka hiyo ya 90 ndio dunia ilishuhudia mauaji mengi ya wasanii wanaofanya muziki huo.2pac kabla hajauwawa alikuwa  tayari amesharekodi wimbo wa "Do for love" uliopatikana kwenye albamu yake ya "R u still down? (Remember me) lakini haukuwa na video.

Bill Parker kwa kushirikiana na Nichole Graham walipata fursa ya kutengeneza video hiyo kwa mtindo wa kikatuni kwa kutumia mbinu za 2D,3D animation,Claymation stop-motion na nyinginezo.Mbali na "Do for love" hakuna video nyingine ya 2pac iliyowahi kutengenezwa kwa mtindo huu.
.
.

No comments:

Post a Comment

Active Visitors

Pages