CHARLES SCHULZ ANATENGENEZA HELA AKIWA KABURINI

**  **

Charles Monroe Schulz ni msanii wa katuni aliyejijengea heshima kubwa katika taifa la Marekani.Baraza la seneti lilipitisha muswada wa kumtunuku medali ya dhahabu ( Congressional Gold Medal ).Juni,20 mwaka 2000 raisi Bill Clinton alitia sahihi kwenye muswada huo na kuridhia atunukiwe medali hiyo.katika kipindi chote cha maisha yake ya kisanaa mpaka anafariki mwaka 2000 alikadiriwa kuwa na utajiri wa dola za kimarekani bilioni  $1.1 ambazo ni zaidi ya trilioni 2 za kitanzania.Jarida la Forbes limekuwa likimtaja kila mwaka miongoni mwa watu maarufu waliokufa wanaoingiza kiasi kikubwa cha fedha na tangu mwaka 2000 hadi leo hii hajawahi kukosa 10 bora.Mwaka 2016 aliingiza dola milioni $48,alishika nafasi ya pili nyuma ya Michael Jackson aliyeingiza dola milioni $800.Watu wengine maarufu ambao wamekuwa wakiingia na kutoka katika orodha hiyo ni pamoja na hayati Bob Marley,Tupac Shakur na mwanasayansi Albert Einstein.

No comments:

Post a Comment

Active Visitors

Pages