THE CROODS - HATUWEZI KUFANIKIWA BILA KUBADILI FIKRA ZETU

** **

Nilipata nafasi ya kutazama mahojiano ya msanii wa katuni maarufu wa hapa nchini Nathan Mpangala akieleza maana halisi ya katuni.Katika maelezo yake aliielezea katuni kama chombo cha mawasiliano kinacho kusudia kufikisha ujumbe kwa jamii husika,pia mbali na kufikisha ujumbe ni lazima iburudishe.Kwa maana hiyo katuni ni chombo cha kufikisha ujumbe husika kwa njia ya kuburudisha.Hii ndiyo imebeba dhana kuu ya mada yetu ya leo kuhusu "The croods".The croods ni filamu ya katuni iliyotengenezwa na kampuni ya "DreamWorks Animation",hii ni filamu ya kwanza kutoka DreamWorks Animation kusambazwa na kampuni ya "20th Century Fox" baada ya "Paramount Pictures" kumaliza mkataba wao.The croods ni familia inayojumuisha watu 6,familia hiyo iliishi mapangoni maisha ya taabu na hofu kwa kuwakimbia wanyama wakali wasiwadhuru.Fikra zao zilijengwa kwa mtazamo hasi kuwa "jambo lolote jipya ni baya",waliamini kuwa mambo yote mapya ni hatari kwa mustakabali wa maisha yao.Waliendelea kuishi kwa mazoea maisha ya hofu hadi pale alipokuja mtu wa kuwapa changamoto mpya zilizowaamsha usingizi mzito waliokuwa wamelala.Pale walipobadili fikra zao maisha yalibadilika na ghafla wakaanza kuishi maisha ya furaha hata wale wanyama wakali waliowakimbia mwanzo waligeuka na kuwa rafiki zao.Lazima ileweke "Hatuwezi kufanikiwa bila kubadili fikra zetu" huo ndiyo ujumbe tunaoupata kwenye filamu ya "The croods".Ilitengenezwa kwa bajeti ya dola za kimarekani milioni $135 na mauzo yake ulimwenguni kote yalikuwa dola milioni $587.2.Kwa mara ya kwanza ilizinduliwa nchini Ujerumani kwenye tamasha la 66 la Berlin International Film Festival.Nyota wa filamu za mapigano wa nchini Marekani "Nicolas Cage" aliingiza sauti yake kwenye filamu hii ya "the croods",aliigiza kama muhusika mkuu,alitumia jina la "Grug".Nicolas Cage anajulikana zaidi katika filamu yake ya "Ghost rider".

No comments:

Post a Comment

Active Visitors

Pages