"Well,John,your project is now complete,so your employment with the Disney studio is now terminated".
Hii ni kauli aliyoambiwa msanii wa katuni John Lasseter na bosi wake siku alipofukuzwa kazi.Kosa kubwa alilolifanya John Lasseter ni kutambulisha katuni za kisasa (3D animation) kitu ambacho kilikuwa sio utamaduni wa kampuni.Kwa vile 3D ni mfumo wa kisasa zaidi pia ulitumia gharama kubwa,kitendo hicho kiliwakasirisha viongozi wake kuona rasilimali za kampuni zinatumika vibaya kwenye kitu ambacho hawajui mwisho wake,hawakupenda kumpa muda zaidi,walifikia uamuzi wa kumfuta kazi.Lasseter hakukata tamaa alibahatika kupata kazi kwenye kampuni nyingine baada ya muda,alifanya kazi kwa mafanikio makubwa na cha ajabu zaidi wale waliomfukuza kazi baada ya miaka 22 walirudi vichwa chini na kumuomba kufanya nae kazi tena pia walimpa cheo kikubwa kwenye kampuni.Somo kubwa unalotakiwa kujifunza ni kuwa siku zote maishani hutakiwi kuvunjika moyo iwapo watu hawakithamini kitu unachokifanya kwa muda huu ni vyema ukaendelea kuamini kuwa ipo siku dunia itautambua uwezo wako.Leo hii John Lasseter ni miongoni mwa wasanii wa katuni matajiri zaidi ulimwenguni akiwa na utajiri wa zaidi ya dola za kimarekani milioni $100 ambazo ni zaidi ya bilioni 200 za kitanzania.
No comments:
Post a Comment