ANGRY BIRDS IMEFANYA AKAUNTI ZA BENKI ZA ROVIO ZIENDELEE KUCHEKA


********************************
"If you haven't accomplish anything you have no right for entertainment", "kama hakuna jambo lolote la maana ulilolifanikisha huna haki ya kuburudika.Bila shaka matajiri au wawekezaji wa Rovio entertainment watakuwa wanaangua vicheko na kugongnisha glasi za vinywaji wakisherekea mafanikio ya "Angry birds.

       Rovio entertainment ni kampuni ya kutengeneza michezo ya kompyuta ya nchini Finland iliyohusika kutengeneza mchezo wa kompyuta wa "Angry birds".Utakuwa unajiuliza kuna uhusiano gani kati ya sanaa ya katuni na michezo ya kompyuta ila ni ukweli usiopingika kuwa sanaa hizi ni sawa na ndugu wanaochangia mzazi mmoja,hili tutalizungumzia kwa urefu zaidi katika makala zangu zinazofuata.

       Kwa sasa "Angry birds ndio mchezo wa kompyuta wenye mafanikio ulimwenguni kote.Umenunuliwa mtandaoni zaidi ya mara bilioni 3 na kuufanya kuwa mchezo ulionunuliwa zaidi katika historia ya michezo ya kompyuta kwa sasa.

       Hayo ni mauzo ya mtandaoni tu bado hatujaangalia ni makampuni mangapi yamenunua leseni za kutumia michoro ya Angry birds kwenye bidhaa zao na vyanzo vingine vya mapato.

       Mimi na wewe hatujui akaunti za benki za kampuni ya  Rovio entertainment zina kiasi gani kwa sasa ila kwa muhtasari huo unaweza kuona ni jinsi gani zinaendelea kucheka na fedha siku baada ya siku,na hiyo ndio imewapa jeuri ya kwenda kuidhamini timu ya "Everton"mbali na "Sportpesa" ambaye ndiye mdhamini mkuu.

         Miongoni mwa watu maarufu wanaopenda kucheza kucheza mchezo huo ni nyota wa NBA Kelvin Durant na waziri mkuu wa zamani wa Uingereza David Cameron ambaye anapenda kuucheza mara kwa mara kwenye Ipad yake.
         Pamoja na mafanikio hayo mkurugenzi mtendaji wa Rovio entertainment Mikael Hed na uongozi mzima wamekuwa wakiumiza vichwa kuona ni namna gani watafanya ili chapa(brand) ya Angry birds iendelee kuwa kubwa ulimwenguni.

************************************

No comments:

Post a Comment

Active Visitors

Pages