Maajabu ya Jiwe MBUJI.
Jiwe mbuji linapatikana Mkoani, Ruvuma, wilayani mbinga katika kijiji cha Litembo, maeneo ya Mbuji.
Hili jiwe ndio jiwe kubwa zaidi mkoani Ruvuma, ambalo lipo toka enzi,kale na kipindi cha apo kale Jiwe hilo lilikuwa linatumika na Mababu zetu,waganga na hata wa chawi kufanya matambiko yao ya mizimu, haya yana simuliwa na wenyeji wa maali apo.
Sasa toka enzi na enzi jiwe hilo ,limekuwa na maajabu/zengwe kadhaa na stori za kutatanisha..Nakumbuka siku ya kwanza niliotembelea Jiwe hilo, mwenyeji alie nipeleka huko,alinisimulia stori ya Wazungu wa wili kufa hapo.
Inasemekana apo nyuma kuna mzungu ambae alitembelea jiwe, hilo na walipo muonya kutokupanda jiwe hilo bila maelezo/baraka za wenyeji alikuwa mbishi, hivyo alipanda na baada ya kupanda punde alidondoka na kichwa kupasuka kisha kufa, japo mwenyeji mwingine aliniambia , baada ya yule mzungu kupanda ,ilidondoka mifupa yake tu.
Kingine nilicho shuhudia na kuhakiki ni Ugumu wa kulizunguka jiwe hilo, ase ilikuwa ajabu, kwasababu tuliweka halama sehemu tulio anzia lakini cha kushangaza tulilizunguka tu ya bila kufikia alama ile, ilituchukua masaa mawili ,ndipo baadae nilipo choka na kushindwa kuendelea, lakini niliambiwa wapo ambao wana weza kulizunguka.
Kingine,chaajabu ambacho nilisimuliwa ni kuhusu Ndondocha,wao wanaita Vibuta, inasemekana katika jiwe hilo, ukipita kuanzia mida ya usiku unaweza ukakutana na Viumbe, vyenye muonekano kama wa binadamu lakini wao uso unakuwa mweupe na huwa wafupi mno, wana waita Vibuta.
pia ukiwa kwa chini jiwe hilo linaonekana kama mlima, lakini ukipanda juu ya jiwe hilo utaona tambalale kubwa kama uwanja wa mpira.
Mpaka sasa sehemu hiyo inaheshimiwa na wenyeji wa apo,pia jiwe hilo linatumiwa kama sehemu ya matambiko kwa waganga na wazee wa mila katika kijiji hicho .
Maajabu ya Jiwe MBUJI.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment