Stephan Bibrowski.
Huyu alizaliwa mwaka 1891,Nchini poland na kufa mwaka 1932 ,nchin Ujerumani alipo kuwa na miaka 41, stephan alizaliwa akiwa na tatizo la Hypertrichosis ,ambalo lilimpelekea kuota nywele zilizo mzunguka mwili mzima, na kupelekea kuwa na muonekano wa kutisha , kama simba.
Kupitia muonekano huo, alikuwa ana fanya maonyesho kwenye matamasha mbali mbali ,hii ilimpelekea kuwa maarufu ,lakini baadae aliacha kazi hiyo baada ya mama yake mzazi kumkataza.
Japo kuwa stephan alikuwa na muonekano mbaya, lakini alipenda kuwa smart mara zote, alikuwa mpole na mtu mwenye akili nyingi, na alikuwa anajua kuongea lugha tano kubwa za dunia.
Alikufa akiwa na miaka 41, baada ya kupata mshtuko wa moyo. ✨✨MWISHO✨✨✨
No comments:
Post a Comment