STEPHEN HILLENBURG - MWANABIOLOJIA ALIYEIKIMBIA TAALUMA YAKE NA KUGEUKIA SANAA YA KATUNI

**
Stephen Hillenburg ni mtaalamu wa biolojia ya viumbe waishio majini (Marine biologist) aliyefundisha katika taasisi ya ORANGE COUNTY MARINE INSTITUTE huko Dana Point,California nchini Marekani.Alipenda kuchora tangu utotoni lakini aligundua ni ngumu kutegemea sanaa kuendesha maisha.Alifanya sanaa ya katuni kama kitu alichokipenda huku akiendelea na kazi yake ya ufundishaji.Ghafla kazi zake zilianza kukubalika,alipokea maombi mengi kutoka makampuni mbalimbali yakimuomba kufanya nae kazi.Aliona huo ndio muda muafaka wa kufanya kitu alichokipenda tangu utotoni.Leo hii ni miongoni mwa wasanii wa katuni waliofanikiwa na anajulikana zaidi kwa katuni yake ya "Spongebob square Pants" inayorushwa kwenye kituo cha luninga cha Nickelodeon.

No comments:

Post a Comment

Active Visitors

Pages