Japo katuni za "Tom and Jerry"zimetengenezwa miaka zaidi ya 50 iliyopita ila kila unapozitazama ni kama zimetengenezwa jana hazijawahi kupoteza radha yake na wala hazionyeshi dalili.
Vipaji maridhawa walivyojaaliwa William Hanna na Joseph Barbera walipokutana katika studio za MGM miaka ya 1950 hii ndio zawadi kubwa waliyotupatia.
Ingawa hatupo nao tena duniani ila wameacha alama isiyofutika kwani kazi zao zitaendelea kukumbukwa vizazi hadi vizazi.Mbali na "Tom and Jerry" kazi zao nyingine ni pamoja na "Scooby Doo" na "Flint stone".
No comments:
Post a Comment