ALIENS IN ZIMBABWE
Katika matukio ya kushangaza kabisa ya karne hii yaliyoacha maswali mengi ulimwenguni kote ni pamoja na tukio la wanafunzi waliodai kuwaona viumbe Wanao dhaniwa kuwa Aliens huko nchini Zimbabwe.
-
Mnamo asubuhi moja ya septemba 16 mwaka 1994 walimu na wafanyakazi wa shule ya ariel walishikwa na mshangao baada ya baadhi ya wanafunzi kuanzia miaka 7 na 12 kudai kuna ndege ya ajabu ilitua katika viwanja vya shule hiyo.
-
Muda huo walimu walikuwa kwenye kikao hivyo wanafunzi walikuwa nje bila uangalizi wowote wakati tukio hilo linatokea, siku mbili kabla ya tukio hilo huko mjini Harare kilomita 20 kutoka mji wa ruwa kuliripotiwa kuonekana vitu vinavyopaa angani visivyoelewka.
-
Watoto hao walidai kwamba mwanzo waliona vitu tofauti vitatu vinazunguka angani baada na ya muda vinapotea na kutokezea tena eneo lingine halafu vyombo hivyo vikaanza kusogea kuelekea chini mwishowe vikatua katika vichaka pembezoni mwa viwanja vya shule hiyo. -
Wanafunzi hao wakadai waliona kiumbe mfupi mithili ya mwanadamu mwenye urefu kama mita moja kasimama juu ya chombo hicho. Ghafla yule kiumbe alianza kuwasogelea wale wanafunzi taratibu. Kimwonekano alikuwa ana shingo kama ya mtu mzee sana, macho makubwa meusi na nywele ndefu nyeusi. -
Ghafla wanafunzi wale walianza kupiga mayowe wakikimbia huku na kuo kuomba msaada wakijua labda ni mashetani waliyokuwa wakihadithiwa na mababu zao katika baadhi ya hadithi. -
Kelele zile zilimshtua kiumbe yule alipowaona wanafunzi wale na ghafla alipotea na kutokeza tena pembeni ya kile chombo ambacho kiliondoka ghafla na kupotelea angani.
-
Cynthia hind mchunguzi wa matukio ya UFO barani africa aliwasili shuleni hapo kesho yake asubuhi ambapo ali kutana na mkuu wa shule hiyo, wanafunzi Zaidi ya 65 waliapa na kuripoti vitu vinavyofanana kuhusu tukio hilo.
waliambiwa wachore picha za kile walichokiona jana yake. Zilichorwa picha tofauti 35 zilizokuwa na mwonekanao wa aina moja.
MMOJA wa watoto hao alisema viumbe hao walikuwa wakitoa ishara kuonesha kwamba binadamu tunaharibu dunia yetu kwa uchafuzi wa mazingira hivyo tuache kabla hakujawa na madhara makubwa
Michoro ile ililingana na mamia ya matukio ya watu waliokiri kuona viumbe wa ajabu duniani
-
Kitabu kimoja kinachoitwa The Report On Identified Flying Object cha mwaka 1955 kilichoandikwa na Ruppelts kimeelezea mamia ya matukio ya kuonekana kwa UFOS duniani kikiandika shahidi mbalimbali za kweli kutoka kwa marubani wa jeshi pamoja na wanasayansi mbalimbali ambao walitoa ushahidi kuhusu kuwaona viumbe hao wakiwa huko angani.
-
Shahidi nyingi zimethibitishwa lakini mpaka sasa kisa cha zimbambwe kimeacha maswali kadhaa,
Lakini Kitu ambacho Kina acha Maswali Mengi Zaidi Ni kwamba wengi ambao Wana fanikiwa kuwaona viumbe hao kwa Ukaribu na kujaribu kuchukua picha Wanaishi kuwa machizi (Matatizo Ya Akili na Saikolojia) Hasa kwa wale walio fanikiwa kuwaona katika Kisiwa cha Triangle Bermuda. -
Hadi Sasa Hakuna Picha Halisi za Aliens ambayo zime wahi kuonyeshwa kwa watu Na wengi ambao Wana fanikiwa kuziona Wana potelea kusiko julikana kwa mfano Bwana Gary Mckinnon.
Picha zinazo onekana Ni za kubuniwa na watengeneza movie pamoja na NASA kwaajili ya Kuficha ukweli na kupumbuza watu. -
Kitu cha Kushangaza Zaidi ni hata wale watoto walio waona ALIENS wakiwa wadogo kule Shuleni Wana Shindwa kutoa maelezo ya kutosha katika ukubwa wao, -
Moja kati ya vitu ambavyo vinatajwa kuwa sababu ya kutotaka kuwekwa wazi picha za Aliens Ni ile Project ya CERN ambapo moja kati ya mikakati yake Ni ALIENS INVANSION.
ALIENS IN AFRICA
STORY
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment