ZOMBIE 2

ZOMBIE -2
Hadithi za Halloween, sherehe inayofanyika kila mwaka mwishoni mwa mwezi wa October (tarehe 31). Hii ni sikukuu ambayo usheherekewa usiku kabla ya ile sikukuu ya watakatifu wote, kwa ufupi halloween ni sikukuu ya wafu (Mizimu). 
Na ilianza miaka 2000 iliyopita uko Ireland, lakini imekuja kuwa maarufu sana kwa nchi za ulaya na haswa ikiusisha uvaaji wa nguo za ajabu ajabu, na uchomaji wa moto na mapambo majumbani.
Mwanzoni ilisemekeana wafu/mizimu walikuwa wakija kusumbuwa watu duniani, na haswa waliharibu mazao, ambayo yalivunwa kipindi cha joto na kuwekwa akiba kwa ajili ya kipindi cha baridi (Winter), sasa ili kuwababaisha wasitambuwe nani ni nani ndio wakabuni haya mambo ya kuvaa kama maiti zilifukuriwa ili kuwachanganya hao magosti.
Lakini wengine wanasema kuwa, uvaaji wa nguo nyeusi misibani ni kweli unatokana na utamaduni wa kimagharibi, na haswa Roma ya kale, (ancient Rome), wao walikuwa wakivaa aina ya nguo inayojulikana kwa jina la toga, ni aina ya shuka ndefu nyeusi inayokadiriwa kufika futi 20 (6 m) kwa urefu wake. Ambayo uzungushwa mwilini, toga ilivaliwa na wanaume na wanawake walivaa stola.
Na wengine wanasema kuwa chanzo cha nguo nyeusi kuvaliwa msibani ni pale malkia Victori, alipokuwa akiomboleza kifo cha mumewe alikuwa akivaa nguo nyeusi tu na alivaa kwa muda mrefu sana... Hii ilipelekea raia nao kuvaa kila wanapopata msiba ya watu wanao wapenda.
Kwa hali ya kawaida zombie hawapo sababu maiti inapo fanyiwa Post Mortem Decomposition ina haribu muonekano wa mwili. 
Ki biologia mtu hawezi kusimama na kutembea kama hana misuli kwa mfano misuli ya mapaja ikianza kuoza atashindwa kusimama na kupiga hatua ili atembee. 
Itaendelea ⚫

No comments:

Post a Comment

Active Visitors

Pages