ZOMBIE 1
by Imatheboy
Zombie ni neno lililo tokana na lugha ya Haiti (zonbi, North Mundu, nzumbe), wakimaanisha maiti inayo tembea.
⚫
Simulizi za kuwepo kwa Viumbe wa Aina hii zipo karibia tamaduni nyingi tokea tamaduni za kale hata tamaduni za sasa, hapa kwetu Tanzania wanaitwa kwa majina tofauti tofauti kulingana na lugha ya kabila fulani, kwa mfano zombie wanajulikana kwa jina maarufu la ndondocha au msukule.
⚫
Kuna ambao wanajaribu kuwa tofautisha kati ya ndondocha na msukule, wanasema kuwa tofauti kati ya viumbe hivi viwili ni
⚫
ndondocha ni watu walio fanyiwa mambo ya kushirikiana na kubadilishwa akili zao kuwa kama watumwa na wakajikuta wanafanya mambo ya ajabu ajabu.
⚫
Msukule kwa upande mwingine ni watu ambao Wana aminiwa kuwa wamekufa lakini kumbe wame chukuliwa kwa kushirikina ili kumtumikia mganga, mchawi, au mwana mazingara Fulani.
⚫
Msukule ndio hao kwa kwa Kiingereza wanaitwa "Zombie" lakini bado Wana watofautisha kati ya msukule na zombie, wanasema kuwa Zombie kwa utamaduni na hadithi za kimagharibi, yaani nchi za ulaya ni watu walio kuwa wamekufa lakini wakarudi wakiwa nusu wafu na wasio na akili timamu.
⚫
Lakini Msukule ni watu ambao hawajakufa kabisa ila wamefanywa waonekane wamekufa na binadamu wengine.
⚫
Kwa Asilimia kubwa tunacho kiona kwenye filamu za vampire na zombies ni simulizi tu za kutaka kuburudisha watu si mambo ya kweli, japokuwa wanaweza kushabihisha na matukio ya kweli.
⚫
Mawazo ya kufikiria kuwa kuna misukule au zombie ni mawazo ya watu wa zamani , zamani watu wa ulaya walikua Wana amini wafu wana uwezo wa kufufuka na kuja kusumbua watu walio hai,
⚫
Na hii ni kutokana na wivu walio kuwa nao hao wafu, au wakati mwingine hurudi kuja kutafuta haki walizo dhurumiwa na mambo mengine.
⚫
Sasa ili kuwatisha na kuwafanya wasiwe na uwezo wa kurudi ndio kukabuniwa hizi nguo nyeusi ili kuzitisha roho zinazotaka kurudi duniani.
⚫
Karibu kwenye app yetu ⚫Imatheboy ClassicTz
No comments:
Post a Comment