MACHALE (INTUITION)
. Ni ile hali au uwezo wa kujua kitu au kukisia jambo, ya bila kuwa na uhakika, uthibitisho au kuwa na sababu thabiti, pasipo kujua ni vipi umepata akili au hisia hizo na sikuzote machale yana ambatana na uwoga. Katika maisha ya kale, machale yalikuwa yana husishwa kiDini na Matendo ya kiroho mfano ,Meditation. Lakini, uhalisia Machale ,ni mawazo ya ndani kabisa (inner feeling au gut feeling), ambayo yana ambatana na ubongo, katika kuchakata taarifa ya bila wewe kujitambua. Machale, ni zawadi ya kila mmoja, lakini wengine wana puuza sanaa yale mawazo ya ndani kabisa. Mfano, utakuta mtu labda unapiga pasi, na unataka kuongeza moto,lakini mawazo yanakujia kwamba nikiongeza moto apa nguo ita ungua, lakini unapuuza unaongeza moto, na kweli nguo inaungua unabaki kujilaumu. Machale sikuzote yamekuwa na muungano na mambo mazuri au mabaya, mfano Kifo, ajari, mafanikio, ushindi n.k. Machale sikuzote yana leta majibu kwanza kabla ya tatizo au jambo lenyewe, mfano. unaweza ukawa unapita njia flani,lakini yanakujia mawazo ya kusema kwamba , Nitavamiwa huku mbele, lakini hujui ni vipi utavamiwa na kweli unaweza ukaenda na ukavamiwa kweli na utajua sasa vipengele vyote vya kuvamiwa. Machale yana uwezo wa kukujia ya bila wewe kujitambua, mfano, Unasafari kesho saa kuminambili asubuhi, lakini iyo kesho usingizi ulikushika na ukachelewa safari na gari lina kuacha ,unabaki kulia, lakini baada ya muda kupita unasikia taarifa kuwa lile gari limepata ajari na wote wamekufa, lakini wewe pekeako umepona kwasababu ulichelewa gari. Machale yana uhusiano na maisha ya liyo pita, sasa, na yajayo, kupitia maisha ya kila siku. kwa ujumla kila unacho kifanya ubongo una kihifadhi na sikuzote ubongo una uhusiano na gut feeling (mawazo ya ndani), sasa hisia ikikujia kuhusu tukio fulani ubongo moja kwa moja unalifanya liwe tukio la kweli ambalo, linaenda kutokea iwe ukweli au uwongo. Machale yana weza kuwa ukweli au uwongo, na sikuzote ili kuwa karibu na machale yako inakuitaji uwe mtu makini sana katika kuyafuatilia mawazo yako, hisia , ndomana watu wanaojihusisha na mindfulnes , mfano Meditation, wanakuwa na machale sana kwasababu ya umakini wa hisia zao. ✨✨END✨✨

No comments:
Post a Comment