EMOTIONAL PAIN ( MAUMIVU YA KIFISIOLOJIA)

EMOTIONAL PAIN ( MAUMIVU YA KIFISIOLOJIA)
Siku zote katika maumivu (Pain) , yapo ya aina mbili, ambayo ni Physical pain(maumivu ya kawaija) na Emotional pain( maumivu ya hisia). Physical pain, haya ni maumivu, dalili zake huwa ni wazi kabisa, mfano , maumivu unayo yapata kutokana na Kidonda, uvimbe au kuvunjika, na siku zote haya maumivu huwa uponywaji wake ni rahisi ni kufuata tu taratibu zinazo hitajika.
Tuachane na hayo, makala hii ina husu Emotional pain, ambayo haya maumivu yame kuwa ni hatari sana kwasababu yana madhara kuliko physical pain.
Emotion pain, hii ni aina ya maumivu ambayo, kila mmoja inamkuta na aina hii ya maumivu ina husisha hisia za ndani kabisa, yani Nafsi, ambapo kwa lugha laisi watu huita Maumivu ya moyoni.
Aina hii ya maumivu haina ile dalili ya kuonekana moja kwa moja, mfano labda ukamtazama mtu na kumgundua kuwa ana emotional pain, bali maumivu haya dalili zake zina hisiwa na muhusika pekee.
Mfano , wa emotional pain, nipale labda mtu una mke au mume wako unae mpenda lakini inatokea siku unakuja kujua kuwa anakusaliti au anakuacha kwa dharau, sasa ile hali unayo ipata ndani ya nafsi yako, ambayo moja kwa moja inaharibu kabisa mfumo mzima wa fikra, na kukufanya ujenge kisilani, malipizi , chuki, au kukata tamaa n.k, ndio emotional pain yenyewe.
Emotional pain, huwa ipo kwa kila mtu kutokana na mazingira husika ya mtu huyo, kwa mfano, ni mbaya sana kwa mtu mwenye, hasira, muoga, mwenye kupenda kuweka kisasi, mwenye chuki na hata mwenye kisirani.
Na imotion pain ,ni moja ya kisababishi kikubwa cha vifo Duniani, na sikuzote maumivu haya yaki mpata mtu mwenye hasira + chuki na kisasi, madhara yake ni makubwa sana, mfano, Mtu anakosewa lakini akiwa na emotional pain kubwa, ana uwezo wa kuua, lakini baadae punde maumivu yanapo kwisha akajuta.
Vifo vingi vinavyo tokana na mapenzi, stress , mshtuko n.k huwa ni matokeo ya emotional pain, na siku zote kuyazuia haya maumivu ni vigumu, kwasababu yapo ndani ya nafsi yako. ITAENDELEA, usikose kujua jinsi ya kujizuia pindi unapokuwa katika haya maumivu

No comments:

Post a Comment

Active Visitors

Pages