Ronald aikumbuka Apple Inc

Ronald Wayne alikuwa mmoja wa waanzilishi watatu wa kampuni ya Apple Computers (Apple Inc kwa sasa). Baadae aliziuza hisa zake zote ambazo zilikuwa sawa na 10% ya mali za kampuni kwa dola 800, kisha wenzake, Steve Jobs na Steve Wozniak wakamlipa dola 1500 zaidi ili asije akaanza kuwadai baadaye. Jumla alipata dola 2300 kwa hisa zake zote. Kama angekuwa nazo hadi leo, hisa hizo zingekuwa na thamani ya dola bilioni 100.

No comments:

Post a Comment

Active Visitors

Pages