Hii nifamilia tajiri zaidi duniani toka karne ya 19 ,mpaka sasa karne ya 21. Mtu wa kwanza kujulikana na jina hilo la Rothschild alikuwa ni Izaak Rothchilid mwaka 1677, ndie baba wa mwanzilishi wa Familia hiyo kubwa ya kibiashara Duniani.
Rothschild family ilianzishwa na Mayer Amschel Rothschild ,alie zaliwa mwaka 1744 na kufa mwaka 1812, ambapo alianzisha hii familia ya kibiashara baada ya kuanzisha benki miaka ya 1760s, katika mji wa Frankfurt ,Ujerumani kupitia jina hilo la rothschild.
Familia hii asili yake ni Ugerumani ,katika tamaduni ya kijewishi, sasa baada ya Mayer Rothchilds kuanzisha Benki, na kuwa na mafanikio mazuri, ndipo alipo kuja na mpango wa kuanzisha Banki hizo nchi mbali mbali duniani yan "benk za kimataifa" kupitia watoto wake.
Watoto wake walisambaa nchi mbali mbali ikiwemo Mji wa london, Paris,Vienna na frankfurt ambapo katika watoto wake alio watuma ,akiwemo Sir. Nathan Rothschild (Uk), James Rothschild(paris), Carl rothchild(Austria) n.k.
Baada ya kuanzisha Benki hizo, familia ilikuja juu sana, na kuwa ndio watu wa kwanza kuanzisha mifumo ya kibenki duniani (International financing system), hivyo watu wengi walio fungua matawi ya benki walikuwa wanahudumia kupitia mifumo ya hawa jamaa.
Katika karne ya 19, walifanikiwa sana hivyo wakawa ndio wanao endesha mabenki makubwa,kalibia yote ya Dunia,kupitia wanafamilia hao ambao walikuwa wamezunguka Nchi kubwa zilizo kuwa zimeshikiria uchumi wa dunia kipindi hicho.
Sasa kadri familia ilipo kuwa inazidi kuongezeka yan vizazi kwa vizazi ndipo ,utajiri wa familia hii ulipo kuwa unazidi kuongezeka, ikawa kila uzao mpya ukitokea basi yule mtoto ana andaliwa sehemu ya kuendeleza gurudumi la biashara katika familia hiyo.
Ilifika kipind hawa rothschild family walikuwa top,yani ukizungumzia benki yeyote duniani , ilikuwa una wataja hawa jamaa,sasa baada ya kuona wameishika dunia katika mifumo ya kipesa, sasa wakaingia katika nyanja nyingine tena, ambapo walianza kumiliki Migodi mikubwa duniani, Nishati, Kilimo na uanzishaji wa viwanda vikubwa vya utengenezaji wine.
Rothschilds walianzisha Familia Kubwa nne ambazo ... ✨✨ITAENDELEA✨✨
No comments:
Post a Comment