HYPERTRICHOSIS Ni uotaji wa nywele uliopitiliza

HYPERTRICHOSIS
Ni uotaji wa nywele uliopitiliza na usio wa kawaida kwenye mwili usiotegemea umri,jinsia wala asili ya binadamu husika. Hali hii inaweza kutokea kwenye mwili mzima
.
Tatizo hili linaweza kutokea kwa mfumo wa kurithi wakati wa kuzaliwa au hutokea tu wakati wa kipindi chochote cha maisha ya binadamu Kutokana na kuongezeka kwa jinzi(genes) zinazochochea ukuaji huo wa nywele. Tangu zama za kati za mabadiliko ya binadamu kuna watu 50 tu hadi sasa walioripotiwa kukabiliwa na tatizo hili.
.
Msingi wa matibabu yake hulenga kuondoa nywele zilizopo mwilini. Njia nyingi zimekuwa zinatumika lakini inahitajika kurudia mara kwa mara sababu nywele huendelea kuota. Mfano wa njia hizo ni kama vile kunyoa kila mara, chemical epilation,electrolysis &thermolysis pamoja na waxing. Katika siku za hivi karibuni uondoaji nywele hizi kwa njia ya miale (Laser hair removal) imependekezwa kuwa miongoni mwa njia za kukabiliana na tatizo hili. Huwa na madhara machache pia nywele hukawia sana kuota ikilinganishwa na njia zingine

No comments:

Post a Comment

Active Visitors

Pages