WAMI THERESA NTARE.(MALKIA WA WAHA)
Mwami Theresa Ntare Alizaliwa Mnamo Mwaka 1922, Alikua Ni Mtoto Wa Chifu Ntare Huko Heru (Kigoma). Theresa alipata Nafasi Ya kwenda Kusoma Ulaya Sababu Zaman Kulikuwa na Nafasi Maalumu Za Watoto Wa machifu.
Inadaiwa Alikua Ni mtoto Wa Kike Pekee kwa chifu ntare . Ulaya Alisomea Sheria Na Katika Harakat Za Kudai Uhuru Alikua Na Msaada Mkubwa Hasa Katika Mikataba Ya Kimataifa.
Mama Huyu Alitawazwa Kuwa Chifu baada ya Baba yake Kukosa Mtoto Wa Kiume Na Baadae Sasa Alitafutiwa Mchumba Ili Aolewe , mchumba Huyo alitoka Manyovu Sehem moja inaitwa Kalinzi Huko Huko Kigoma.
Sasa Katika Mila za Kiha Mwami Hua Haolewi na akiolewa inabidi aihame Miliki yake ya uchifu ili akawe mke . Familia ya mwami ntare Ililipa mahari Kwa Familia ya Bwana George Shinganya (mume wa theresa) Baada Ya Kufanya Hivo Jina la Shinganya Likafutwa na Kuwekwa Ntare Hivyo Aliitwa George Ntare Ambaye Alitoka Katika ukoo Wa Chifu Lusimbi. Baadae Waliachana Na Akaolewa na Mwami Louis Dantes Kutoka Asili ya Ufipa .
Katika Zama Hizo Jamii Nyiingi sana Za Kiafrika Zilitajwa kuwaweka Nyuma sana Wanawake Hasa Katika Masuala Ya Uongoz Na elimu Hali iliyomfanya Mwami Ntare Ashindwe Kuongoza Kishupavu Jamii Yake Ya Waha . Alikua Pia Ni Mkuu wa Machifu Wote Tanganyika Baada Ya Aliyekuwa Chifu Mkuu Chifu Petro Itosi Marealle.
Aliheshimika Kama chifu Wa Kasulu Yoote Akiwa Mmoja Wa Wabunge Wa Baraza La Kutunga Sheria Tanganyika Kabla Ya Uhuru Hadi Miaka ya 1980. Disemba 9 mwaka 1962 Aliacha Uchifu Katika Uwanja Wa Uhuru Jijini Dar Es Salaam Huku akikaribishwa Kama Malkia Wa Heru.
Katika Shule Ya Secondari Mzumbe Kuna Bweni Moja Huko Linaitwa NTARE hii Ni Kutokana Na Makabidhiano Ya Uchifu Wa Tanganyika Yalipofanyika Huko. Theresia Ntare Alifariki Mnamo Mwaka 1999 Na Kuzikwa Kigoma Sehemu aliyokua akiitawala (Heru Juu). Hiyo ndio Historia Fupi Ya Mwami Ntare Kwa Wale Waliobahatika Kufika Ujiji Makumbusho Ya Living Stone Kuna Historia Ya Mwami Ntare
Historia Fupi Ya mtoto wa chief Mwami Ntare
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment