AKODESSAWA FETISH MARKET.

AKODESSAWA FETISH MARKET.
Hili ni Soko Linapatikana Huko Afrika Ya Magharibi Lome, Togo Katika Wilaya Moja Inayojulikana Kama Akodessawa , Soko Hili Maarufu Watu Huliita Soko La Uchawi Na Ushirikina . Katika Soko Hili Lipo Tofauti Kidogo Na Masoko Mengine Tuliyoyazoea Maana Huko Wanauza Vitu Ambavyo Sio Rahisi Kupatikana Katika Hizi Soko Za Kawaida.

Badala Ya Kuuza Nyanya , Vitunguu ama Mchele Basi Katika Soko Hili Huwa Kumejaa Na Wanauza Mafuvu Na Ngozi Za Viumbe Mbalimbali Kama Nyani Mamba, Mafuvu ya Ndege na Vingine Viiingii. Yaan Product Za Wanyama Na Ndege Waliokwisha Kufa Ndo Hupatikana Huko na Maisha Yanasonga Kama Kawaida.

Katika Soko Hilo Watu Mbalimbali Hufika Na Kujipatia Mahitaji Yao Kama Kawaida Na Wengine Hufika Kwaajili Ya Kuweka Sawa Mambo Yao Na Wengine Hufika Kununua Kabisa Mahitaji Kwaajili Ya Shughuli Zao Mbalimbali. Watu Wengine Hufika Sokoni Hapo Kwaajili Ya Kuondoa Mikosi, Kuweka Sawa Mambo Yao Ya Mapenzii Mfano Unaweza Fika Sokoni Ukajielezea Matatizo Af Unapewa Kamfupa Ka Mnyama Yoyote Na Maelekezo Jinsi Ya Kufanya

Soko Hili Hufurika Sana Wakati Wa Kampeni Za Siasa Na Kuelekea Uchaguzi Maana Viongozi Mbalimbali Hufika Sokoni Hapo Kwaajili Ya Kuweka Mambo Yao Sawa Wengine Hata Kupiga Ramlii Kwaajili Ya Mambo Yao Ya Kisiasa. Wanasema Msimu Huo Viongozi Huwa Wengi Wanaotembelea Katika Soko Hilo.

Ukiachana Na Waganga Wa Jadi Ambao Wao Wamezoeleka Katika Soko Hilo kwa Kununua Vifaa Vya Kazii Lakini Pia Soko Hili Limekua Ni Kivutio Kikubwa Cha Watalii Kutoka Sehemu Mbalimbali Kuja Kushuhudia Soko Hilo Wanalodai Ni La Imani Na Kishirikina. Hivyo Limekua Likichangia Kipato Kwa Serikali Kutokana Na Kutembelewa Na Watalii.

No comments:

Post a Comment

Active Visitors

Pages