PART 2; EYE GAZING......

Kama nilivyo ongelea katika makala iliyo pita , kuhusu hatua za kufanya EYE GAZING.

Baada ya kuwa huru kila mmoja , msogeleane kisha muangaliane machoni kwa ukaribu, apa mtapata vishawishi vya kupepesa macho, msijali, hata kama ukipepesa macho,wew kuwa makini na fikra zako ziwe katika jambo hilo.hakikisha unapo muangalia mwenzoko uone sura yako machoni pake.

Inachukua muda wa takika 7-10, ndipo hali ya utofauti itakapo kuja machoni penu, utaona mwanga unafifia na kutokea kitu kama ukungu hivi , usi shangae wala kushtuka hiyo hali ni ya kawaida ,endeleeni kufocus katika jambo hilo.

Baada ya muda, Utaona , ule ukungu unapotea na mwanga kuludi haraka machoni, na utayaona macho ya mwenzako yana mwangaza kama taa..usiogope wala kushtuka endelea kumwangalia.

Baada ya hatua hiyo, Utaanza kuona picha , mfano wa sinema, na fikra/akili yako ndio itakuwa ina control matukio yote, kwa maana hiyo chochote utakacho kifikili kwa muda huo kuhusu jambo fulani ambalo ulilifanya au mlilifanya katika nyakati zilizo pita, litaonekana hapo, hivyo itakufanya uone hata mengine ambayo hauku ya ona wakati huo , yote yanayo onekana na yasiyo onekana.

Hakikisha mkisha maliza , kufanya hilo jambo ni vyema kila mmoja akamueleza mwenzake yale aliyo yaona.

MATOKEO YA KUFANYA EYE GAZING.

Inajenga au kuharibu Uwaminifu; Hususani kwa wapenz,rafiki au ndugu, punde mtakapo ifanya hii inaweza kujenga uaminifu endapo kama utaona mema ya mwenzako kwako au kuharibu uaminifu kama utaona mabaya yake kwako.

Hii inasaidia kujua mambo mengi sana yanayo kuzunguka , katika nyakati tofauti kupitia kumbukumbu ,hivyo kukufanya upange maisha yako katika mtiririko unao endana na nyakati hizo, na kukufanya ujue katika nyakati fulani unatakiwa ufanye nini .

Inatengeneza mshikamano, ushirikiano na muungano(strong connection) wa karibu, baina yenu, kwa kuwafanya mjuane vizuri zaidi hivyo kutengeneza hisia kali katiyenu mfano, furaha au uzuni.

Itawafanya mfurahi au kuhuzunika , baada ya kuona kumbukumbu fulani za matukio yenu ya kupendeza au matukio ya kuhuzunisha.

pia inajenga kujiamini(consiousness), na kuondoa aibu na uwoga baina yenu au katika jambo fulani. ✨✨MWISHO✨✨

No comments:

Post a Comment

Active Visitors

Pages