Alfajiri ya Septemba 2 1944, ndege ya kivita ya Marekani iliyokuwa inaenda kuangusha mabomu kwenye mnara wa mawasiliano wa wajapan katika kisiwa cha Chichi Jima ilipigwa risasi na kuanza kupoteza uelekeo, lakini rubani wake aliweza kufika sehemu husika na kuangusha mabomu. Watu waliokuwa pamoja naye walikufa baada ya ndege hiyo kuanguka, rubani pekee aliruka na kuangukia baharini. Aliokolewa na boti ya kivita. Rubani huyo alikuwa George H.W Bush, rais wa 41 wa Marekani (1989 - 1993)
Je, Wajua? Akiwa rubani wa ndege za kivita, George H W Bush, rais wa 41 wa Marekani alinusurika kifo mara mbili kwenye vita kuu ya pili ya dunia.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment