Jamais Vu hii ni kinyume cha Déjà vu', kwa Kifupi sana Déjà vu' Ni ile hali ambayo ina tokea unapo fika sehemu Una hisi kama Ulisha Wahi kufika lakini kiuhalisia hauku wahi kufika au Una muona mtu ambaye Una hisi ulisha wahi kumuona lakini kiuhalisia haukuwahi kumuona. -
Tuki rudi kwenye JAMAIS VU hii ni ile hali ya kusahau kitu ambacho Una kiona kila wakati (Mara Nyingi) Unakua Una hisi kama haukifahamu au hauja wahi kukiona Au kigeni lakini kipo akilini kwako. -
Yaani Kwa Mfano Una Fungua Mlango Kila Siku Lakini Ukiulizwa hicho unacho kifungua Ni nini? Una Shindwa kusema huu Ni mlango lakini akili yako ina fahamu kabisa kuwa huu Ni mlango. -
Au Una Kutana Na Mtu Una Fahamiana Nae Kabisa Una Onana Nae Kila Siku Lakini ukiulizwa jina Lake Una shindwa kulitaja, Ingawa akili yako ina fahamu kabisa huyu mtu Ni Nani. -
Pia, Kwa Mfano Una Ambiwa Andika Neno "THANKS" Una shindwa Kuliandika ingawa kwenye akili yako Una Fahamu Kabisa jinsi Linavyo andikwa na wakati mwingine una andika kwa usahihi kabisa lakini akili yako ina kuambia sio hivyo. -
Nimalizie Mfano Wa Mwisho Hapo Ulipo Una weza kujaribu Sema Haraka haraka "Deo, Deo, Deo" Sema Mara 10, Itafika kipindi Masikio Yako yata Sikia Una Sema "Ode, Ode, Ode" ingawa akili yako ina fahamu kama Una sema Deo hii ndo JAMAIS VU. -
Ebu Niongeze Na Hili "Presque Vu" kwasababu Lina fanana na Jamais vu, Presque vu hii ni ile hali ambayo Una kumbuka /fahamu kitu lakini Una shindwa Kukisema, kinakujia kabisa akilini lakini unapo inua Ulimi ili ukitamke ghafla kina potea kibaya zaidi Unapo sema ukumbuke tena ndo kina potea kabisa na uki kumbuki tena, Mara Nyingi ina tokea zaidi kwenye kuongea. -
Pia Kuna "Déjà Entendu" hii ina fanana na Déjà Vu lakini hii kwenye kusikia tu yaani hali ya kusikia sauti ambayo Una hisi ulisha wahi kuisikia lakini ukweli Ni kwamba hauja wahi kuisikia au Una sikia wimbo Fulani Una hisi ulisha wahi kuusikia lakini kiuhalisia haukuwahi kuusikia.
Jamais Vu '
STORY
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment