Mnamo mwaka 1963, mtu mmoja , hakutajwa kwa Jina , alikuwa ana ishi nchini , Uturuki katika mji wa Nevsehir province.
Alikuwa amejenga nyumba yake, kwenye mwinuko/kilima..ambapo alikuwa amechimba upande kidogo wa mlima huo kisha kujenga nyumba yake hapo, na kuufanya ule upande wa mlima alio uchimba kama ni ukuta pia.
Aliishi apo kwenye mlima huo na familia yake kwa miaka mingi, ndipo ilipo fika mwaka 1963, akiwa ndani kwake , ukuta wa upande ule wa mlima ulikuwa unanyufa.
Sikuzilipo zidi kwenda nyufa zili zidi, ili mbidi azibe zile nyufa ,sasa alipokuwa katika harakati za kuziba nyufa hizo kwa bahati mbaya alibomoa ule ukuta.
Chaajabu baada ya kubomoa, aliona chemba kama mlango, ndani ya mwinuko huo, alipo ingia , mule ndani ya ile chemba alikuta kordo na kwandani kulikuwa na mji , wazamani ulikuwa umejengwa miaka mingi iliyo pita na ndani walikuta vitu vingi sana vya kale ikiwemo mafuvu ya binadamu , vitabu n.k.. Baada ya kutoa tarifa serikalini, na kufanywa utafiti, waligundua kuwa ni mji wa zamani ulio itwa Derinkuyu( deep well) ambao ulikuwa unatumika kama maficho wakati wa vita.
Mpaka sasa , eneo hilo limekuwa la kitalii na tafiti nyingi kuhusiana na mambo ya kale zina fanyika hapo...
Derinkuyu( deep well)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment