ALIENS IN ZIMBABWE - 1.........

Katika matukio ya kushangaza kabisa ya karne hii yaliyoacha maswali mengi ulimwenguni kote ni pamoja na tukio la wanafunzi waliodai kuwaona viumbe Wanao dhaniwa kuwa Aliens huko nchini Zimbabwe.
-
Mnamo asubuhi moja ya septemba 16 mwaka 1994 walimu na wafanyakazi wa shule ya ariel walishikwa na mshangao baada ya baadhi ya wanafunzi kuanzia miaka 7 na 12 kudai kuna ndege ya ajabu ilitua katika viwanja vya shule hiyo.
-
Muda huo walimu walikuwa kwenye kikao hivyo wanafunzi walikuwa nje bila uangalizi wowote wakati tukio hilo linatokea, siku mbili kabla ya tukio hilo huko mjini Harare kilomita 20 kutoka mji wa ruwa kuliripotiwa kuonekana vitu vinavyopaa angani visivyoelewka.
-
Watoto hao walidai kwamba mwanzo waliona vitu tofauti vitatu vinazunguka angani baada na ya muda vinapotea na kutokezea tena eneo lingine halafu vyombo hivyo vikaanza kusogea kuelekea chini mwishowe vikatua katika vichaka pembezoni mwa viwanja vya shule hiyo. -

Wanafunzi hao wakadai waliona kiumbe mfupi mithili ya mwanadamu mwenye urefu kama mita moja kasimama juu ya chombo hicho. Ghafla yule kiumbe alianza kuwasogelea wale wanafunzi taratibu. Kimwonekano alikuwa ana shingo kama ya mtu mzee sana, macho makubwa meusi na nywele ndefu nyeusi. -
Ghafla wanafunzi wale walianza kupiga mayowe wakikimbia huku na kuo kuomba msaada wakijua labda ni mashetani waliyokuwa wakihadithiwa na mababu zao katika baadhi ya hadithi. -

Kelele zile zilimshtua kiumbe yule alipowaona wanafunzi wale na ghafla alipotea na kutokeza tena pembeni ya kile chombo ambacho kiliondoka ghafla na kupotelea angani.
-
Cynthia hind mchunguzi wa matukio ya UFO barani africa aliwasili shuleni hapo kesho yake asubuhi ambapo ali kutana na mkuu wa shule hiyo, wanafunzi Zaidi ya 65 waliapa na kuripoti vitu vinavyofanana kuhusu tukio hilo. 
waliambiwa wachore picha za kile walichokiona jana yake. Zilichorwa picha tofauti 35 zilizokuwa na mwonekanao wa aina moja. -

Itaendelea -

No comments:

Post a Comment

Active Visitors

Pages