ROGUE WAVES.
. .
Mawimbi ya mwamba, pia hujulikana kama mawimbi ya kushitukiza, mawimbi ya kustaajabisha, mawimbi ya machafuko, mawimbi ya mauaji, mawimbi yanayodumu, na mawimbi yasiyo ya kawaida, yasiyo tarajiwa na hutokea ghafla yanaweza kuwa hatari sana, hata kwa meli kubwa kama zile za kubeba shehena (cargo of amminition). . .
Mawimbi ya mwamba husababisha hatari kubwa kwa sababu kadhaa:ni makubwa, hayatabiriki, yanaweza kuonekana ghafla au bila ya taarifa, na yana tokea yakiwa na nguvu kubwa.
Pindi yanapo tokea yana uwezo wa kupanda juu kwa urefu wa kuanzia mita 12 (39 ft) hadi mita 18.3 (60ft) kwa kawaida shinikizo la Rogue ni tani 6 kwa kila mita ya mraba [t / m2] (8.5 psi). Ingawa meli za kisasa zime tengenezwa na uwezo wa kustahimili wimbi la Rogue lenye tani m2 (21 psi), lakini wimbi la Rogue linaweza kusambalatisha meli hiyo na takwimu kwa shinikizo la 100 t / m2 (140 psi).
.
Miongoni mwa taarifa za uchunguzi, mawimbi ya rogue huelezwa kwa usahihi kama mawimbi ambayo urefu wake ni zaidi ya mara mbili ya urefu wa mawimbi makubwa ya SIGNIFICANT WAVES HEIGHT (Hs au SWH), Ambapo SWH hufafanuliwa kama ni mawimbi makubwa mara ya tatu zaidi ya mawimbi makubwa kutokae katika rekodi ya mawimbi, una weza ukapata picha ina kuaje pindi yanapo tokea.
Mawimbi ya rogue sio lazima yawe mawimbi makubwa kwenye kila maji maji; lakini ni makubwa pindi yanapo tokea kwenye bahari. .
Mawimbi ya Rogue hayatokei kutokana na sababu moja, kuna sababu tofauti, hutokea kutokana na sababu kama vile upepo mkali, miamba yenye nguvu husababisha mawimbi kuungana na kuunda wimbi moja la kipekee. .
Mawimbi ya juu ya maji ya wazi, ambapo upepo huyakusanya pamoja, mikondo, matukio yasiyo ya mstari kama vile mawimbi yanayo safiri kwa kasi (solitons/quantum Energy) na hali nyingine. .
Pia Mawimbi ya Rogue yanaweza kutokea katika maeneo mengine tofauti na kwenye maji.
Yajue Mawimbi ya bahari " ROGUE WAVES."
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment