TRIANGLE BERMUDA - 1
-
Moja kati ya vitu vinavyo gonga vichwa vya watu Ni sehemu hii ya Triangle Bermuda Maarufu kama Lango la kuzimu eneo hili lina kadiriwa kuwa sehemu hatari zaidi kwa wasafiri wa majini na Angani -
Tangu mwaka 1945, zaidi ya meli 100 zimeshazama na vifo vya watu zaidi ya 1,000 vimeshatokea katika eneo hili ambalo ni maarufu sana kwa vyombo vya safari kupita. Pia ni eneo ambalo linasifika sana kwa kubadilika kwa hali ya hewa kwa haraka na bila kutarajiwa.
Matukio mengi yalitokea katika kipindi cha miaka ya 1940 - 1960, nayo yalihusu upoteaji wa kiajabu wa vyombo vya usafiri hasa ndege na meli.
Mwaka 1944, Dick Stern alikuwa anaruka na ndege ya kivita eneo hili, ghafla ilipoteza uelekea kwa muda na ikawa inaelekea kuanguka Bahari ya Atlantiki, lakini baadaye iliweza kutulia yeneyewe na kuendelea na safari vizuri. Na katika miaka ya 60 alipita tena eneo hilo akiwa na mkewe katika ndege ya kawaida wakapata msukosuko mkubwa.
Kwenye miaka ya 1945, 1958, 1964 na 1967 kuna ndege zilipotea tena katika eneo hilo ambapo mabaki yake hayakuweza kupatikana kabisa. Kuna baadhi ya marubani ambao waliwahi kuripoti kabla ya kupotea au kuokoka kwamba rada zao zilikupoteza uelekeo na kiasi kwamba wakashindwa kujua wako wapi, kuna mmoja aliripoti kuongezeka kwa kasi ya kwenda kwa ndege na kila kitu kikapoteza control, na baadaye vikarudi sawasawa.

Pia kuna rubani mmoja wa ndege ndogo alitaka kutua eneo hilo, lakini alipofika sehemu aliyotaka kutua, hakuiona ilhali watu walio kuwa chini walikuwa wanamuona na kumshangaa akizunguka tu hewani na kisha kuondoka. Baadaye alikiri kuzunguka juu baada ya kutokuona sehemu aliyotaka kutua wakati compass yake ilimuonyesha ameshafika.
Meli amabazo zimekumbwa na misuko sehemu hiyo zimekuwa zikiripotiwa kukutana na mvutano wa ajabu wa kwenda chini na mwishowe kuzama, au kukutana na machafuko ya bahari ya ghafla.
Kuna baadhi ya wafanyakazi wa meli walio okolewa waligeuka na kuwa vichaa!
Kituko kikubwa ni kile kilichoripotiwa mwaka 1967 kutoka kwa watu waliokuwa kwenye meli ya Elizabeth I pale waliposhuhudia ndege ndogo ikiwa mita chache kutoka walipo ikipotea ghafla ikiwa inaruka. -
⚫

No comments:
Post a Comment