Skulls And Bones (01)

SKULLS AND BONES - 1
-
Leo Ebu Tuwa kodolee Macho kidogo Wazee wa mafuvu na Mifupa,
Tarehe 10 February mwaka 2017 ilikuwa ni siku ya kutimiza miaka 100 tangu kifo cha Geronimo ambaye alikuwa ni shujaa kutoka Jamii ya APACHE (hawa ni mashujaa wa wahindi wekundu au wakazi asilia wa Taifa la marekani maarufu kama Red Indians). -
Ndugu mmoja katika jamii hii alifungua mashtaka akiwashtaki Skull and bones  jamii ya Siri ambayo ilianzia Katika chuo kikuu cha YALE huko marekani kuwa iruhusika na kuiba mabaki ya Shujaa Geronimo. 
Miaka kadhaa imekuwa ikipigiwa kelele jamii hii ya Fuvu na Mifupa kuwa imeshikilia mabaki ya Geronimo ikiyatumia kwa shughuli zake za kiimani.
-
Haryln Geronimo (Kitukuu cha Shujaa Geronimo) mwenye miaka 61 anasema “naamini kabisa toka moyoni mwangu kuwa roho ya Geronimo haikuachiliwa” akiwaambia waandishi wa habari walio kusanyika wakifuatilia tukio hili lililo husisha jamii hii ya Skull and Bones. -
Inasemekana kuwa Wakongwe Kama Prescott S. Bush ambaye ni baba wa Aliyekuwa Rais George W. Bush na Babu wa George W Bush  huyu na wenzie wengine wanachama wa Skull and Bones walichimba mabaki ya Geronimo toka kaburini mwaka 1918 wakaiba fuvu la Huyu Shujaa, Na Mifupa miwili na mavazi yake kivita kutoka katika Kaburi lake huko Fort Sill. -
Jamii hii ikachukua mabaki haya na kuyaweka Makao yao Makuu ambayo yalikuwa yame anzishwa toka mwaka 1832.
Kuna mambo mengi ambayo yamekuwa yaki zungumzwa kuhusiana na kundi au jamii hii. Inasemekana hawa ndio walio husika na utengenezaji wa bomu la nyuklia mpaka kuuawa kwa J.F. Kennedy Ingawa Pia Ina semekana Bwana Jf Kennedy alikua ana fahamu Juu ya hicho kifo chake. -

Ni kundi ambalo nchi za huku kwetu hali fahamiki na watu wengi lakini kwa Huko kwa wenzetu ni Kundi kubwa na la kutisha sana. 
Ni Kundi lenye viongozi wakubwa sana duniani likihusishwa na miaka ile lilipokuwepo kundi la mafia kuwa hili ni kundi la mafia la kimataifa.
Pia Wana Patikana Katika Vyuo Vikuu Mbali Mbali Duniani na siku hizi hata Vyuo vya kawaida. -
Itaendelea -

No comments:

Post a Comment

Active Visitors

Pages