Hii ni hali inayo mtokea mtu wakati anapokuwa amelala,ambapo ,unakuwa unaota ndoto,alafu unashtuka ndani ya ndoto, na kukufanya ujihisi upo katika maisha ya kweli/halisi,kumbe wakati huo unakuwa bado unaota na yote utakayo ya fanya yana kuwa katika hali ya ndoto, na unashtuka tena ,ndipo unapo kuja kutambua kuwa kumbe ilikuwa ni ndoto pia.
False awakening,ase hii ni noma na ya maajabu sana, maana unakuwa unaota ndoto mbili kwa wakati mmoja, ambapo ndoto ya kwanza unaota wakati ambao unakuwa katika usingizi mzito na hujielewi, lakini ndoto ya pili unaota wakati ambao unakuwa unajielewa ila hujitambui kama unakuwa unaota, hivyo unahisi upo katika maisha halisi ,kumbe ni ndoto.
Mfano wa False awakening;Nipale mtu unakuwa unaota ndoto na unashtuka ,unajihisi mkojo umekubana una amka na kwenda chooni,kukojoa ,kisha unaludi kulala alafu punde unashtuka na kutambua kuwa kumbe ulikuwa unaota..au unakuwa umelala lakini hujitambui kama unaota,sasa katika iyo ndoto ,asubuhi inafika una amka na unafanya kazizako za kilasiku, alafu punde unashtuka na kutambua kuwa kumbe ulikuwa unaota.
False awakening,huwa ina ambatana na matukio ya ukweli kwasababu unapokuwa katika hali hii unakuwa unahisi upo katika maisha halisi..Mfano. unakuwa umelala alafu unaota ,lakini wewe unakuwa hujitambui kama unaota ,unahisi upo katika maisha ya kawaida ..labda unakuwa na marafiki zako mnatembea ,mnafika sehemu porini, mkojo unakubana ,unatafuta kichaka na unakojoa ,na unapo kojoa unahisi kabisa unakojoa katika maisha halisi ,lakini punde unashtuka na kutambua kuwa ulikuwa unaota lakini sasa ukiangalia godoro limeloa, yani umejikojolea kweli kupitia ndoto...ndo mana unakuta watu wengi wanajikojolea ,kunya au kutapika kitandani wakati ambao wanakuwa wamelala ,ambapo wanota wanafanya vitendo hivyo lakini hawajui kama wanaota wanazani wanafanya katika maisha halisi ,kumbe ni ndoto mwisho wasiku unashtuka unajikuta umejikojolea au umejinyea kitandani ukweli..kumbe ndoto imekudanganya.
FALSE AWAKENING
STORY
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment