Kwa ufupi
Bilionea nchini Tanzania, Mohamed Dewji 'Mo' amezungumza kwa mara ya kwanza baada ya kupatikana akiwa hai
Mo alimepatikana alfajiri ya leo Jumamosi Oktoba 20, 2018
'Mo' Dewji: Namshukuru Mungu
Mohammed Dewji 'Mo'
Mfanyabiashara maarufu nchini Tanzania
Mohammed Dewji 'Mo' anamshukuru Mungu kwa kumrejesha salama.
Mo aliyepatikana alfajiri ya leo Jumamosi Oktoba 20, 2018 amesema hayo kupitia akaunti ya Twitter ya Kampuni ya Mohamed Enterprise Limited (Metl Group).
"Namshukuru mwenyezi Mungu nimerudi salama nyumbani. Nawashukuru Watanzania wenzangu na watu wote kote duniani kwa dua na sala zao."
"Nashukuru mamlaka zote, ikiwemo jeshi la polisi, zilizofanya kazi ya kuhakikisha narudi salama," amesema Mo
Mo amepatikana ikiwa ni siku ya tisa tangu alipotekwa na watu wasiojulikana alfajiri ya Oktoba 11,2018 katika Hoteli ya Collosium jijini Dar es Salaam alikokuwa amekwenda kufanya mazoezi.
No comments:
Post a Comment