Vostok kwa Kirusi Восто́к, ilikuwa jina la mradi wa kwanza wa usafiri wa anga la nje ulio faulu kupeleka binadamu kwenye anga la nje na kuwarudisha tena salama. Ilikuwa mradi wa Umoja wa Kisovyeti ulioshindana na mradi wa Mercury wa Marekani. Mwanaanga Yuri Alexeyevich Gagarin alikuwa binadamu wa kwanza aliyerushwa juu katika chombo cha Vostok 1 tarehe 12 Aprili 1961 na kuzunguka dunia mara moja katika anga la nje kwa kimo kati ya kilomita 315 na 169 na mwisho mwezini. Mradi wa Vorstok ilikuwa na safari sita za kupeleka wanaanga nje ya anga hewa ya Dunia kati ya 1961 na 1963; safari ndefu ilidumu siku tano ambapo Vostok ilimpeleka mwanaanga Valentina Tereshkova aliyekuwa mwanamke wa kwanza katika anga la nje. Mradi ulitumia roketi za kijeshi zilizobeba chombo anga chenye sehemu mbili dambra (chumba kidogo cha rubani)moduli ya huduma (injini, tanki la mafuta, beteri) Wakati wa kurudi wanaanga walirushwa kutoka dambra wakarudi ardhini kwa parachuti.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment