Sputnik 1 (kwa lugha ya Kirusi Спутник kwa maana msindikizaji) ilikuwa satelaiti ya kwanza iliyotengenezwa na binadamu na kuzunguka Dunia katika anga la nje. Ilitengenezwa katika Umoja wa Kisovyeti na kurushwa angani tarehe 4 Oktoba 1957 kutoka kituo cha Baikonur (ambako kwa sasa ni Kazakhstan).
Sputnik 1 ilikuwa na umbo la tufe lenye kipenyo cha sentimita 58 na masi ya kilogramu 83.6. Ilikuwa na antena mbili zenye urefu wa mita 2.4 na 2.9. Ilibeba vifaa vya kupima jotoridi ndani yake pamoja na shinikizo ya gesi iliyojaa mwili wake halafu transmita ya radio iliyorusha vipimo hivi kupitia antena Sputnik 1 ilizungukua Dunia mara 1,440 katika muda wa miezi 3 hadi kushuka na kuungua katika anga hewa ya Dunia tarehe 4 January 1958.
Kurushwa kwa Sputnik 1 kulitokea wakati wa mashindano makali baina ya Umoja wa Kisoveti na Marekani. Marekani ilishtuka kabisa kwa sababu waliwahi kuamini ya kwamba walikuwa mbele. Mshtuko wa Sputnik ulisababisha mabadilio katika siasa ya Marekani iliyoongeza juhudi zake katika teknolojia na elimu. Hapo yalianza mashindano ya anga (Space Race) baina Marekani na Umoja wa Kisovyeti ambako pande zote ziliendelea kupeleka satelaiti nyingi kwenye anga zilizofuatwa na vyombo anga vya kubeba watu.
Mwaka 1961 umoja wa Kisovyeti ulio ongozwa na Urusi ulifanikiwa kupeleka mtu mwezini (Yuri alexeyevich) Marekani ili faulu kufikisha watu mwezini mwaka 1969 (Neil Armstrong). Cha kushangaza kuifuatilia ripoti nyingi zina dai Marekani ndo walikua wa kwanza, pia ripoti za Marekani zina tumika zaidi kuliko ripoti za Warusi ingawa ripoti za Warusi ndo zipo sahihi zaidi. Uhasama kati yao ulianza mda mrefu, Mradi wa UFO ambao una wahusisha sana wamarekani na Warusi ulitegemewa utamaliza uhasama wao lakini matarajio yamekua tofauti. Wachambuzi wa masuala ya ulinzi na usalama wanadai hizo zote ni mbinu zilizo buniwa kwaajili ya kuupumbaza ulimwengu kwani Marekani, Russia na Islaeri ni nchi zenye ushirikiano wa hali ya juu sana.
Ifahamu Sputnik 1
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment