Dunia ya wizi wa pesa za ATM.
Mnamo tarehe 10 Oct, 2014 shirika la polisi kimataifa (Interpol) lilitoa taarifa za kuzitaadharisha asasi za ulinzi na usalama za nchi za Ulaya, Asia, Latin America na Afrika juu ya uhalifu wa wizi wa pesa katika mashine za ATM.
Kampuni ya usalama wa mitandao, Kaspersky wakishirikiana kwa siri na shirika 1 la ujasusi la Urusi walifanya utafiti na kuweza kugundua jinsi ambavyo hackers wanavyofanikisha ukwapuaji wa pesa kupitia ATM. Na hiki ndicho hufanyika kwa nchi nyingi za Magharibi.
Kwanza kabisa hacker anatafuta physical access ya mashine ya ATM, kisha kwa kutumia boot CD ama boot flash anaathiri mfumo mzima wa mashine (hii ni disk maalumu yenye uwezo wa kutunza files zenye memory kubwa sana kwa kufanya mashine isinzie kwa muda).
Baada ya hapo kirusi kiitwa 'Tyupkin' kinaingizwa kwenye mfumo huo wa ATM, kazi ya kirusi hiki ni kukata mawasiliano ya kimtandao kati ya mashine ya ATM na server za benki. Baada ya hapo mfumo wa mashine unaanza kufuata masharti ambayo hacker anaamuru na si instructions za bank.
Mpaka Hapo mwalifu anaweza kuingiza namba za siri ambazo zipo coded tangu awali na kumpa uwezo wa kupakua kiasi chochote cha pesa kilichopo katika mashine.
Njia hii huiba pesa zilizopo kwenye ATM mashine bila kuathiri akaunti za benki za mtu mmoja mmoja. Na pia ni njia inayoitaji ujuzi wa juu sana wa computer.
Hackers wanaofanya wizi wa pesa ATM kwa kutumia Virusi vya 'Tyupkin'
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment