1. Je, wajua kuwa katika ngozi ya mwanadamu mmoja pekee kuna idad kubwa ya viumbe hai kuliko idadi ya wanadamu wote walioko katika ulimwengu mzima?
2. Je, wajua kuwa kama mdomo wako ukiwa mkavu kabisa huwezi kutofautisha ladha mbalimbali?
3. Je, wajua kuwa ubongo wa mwanadamu hutumia zaidi ya asilimia 25 ya oksijeni yote inayotumiwa na mwanadamu?
4. Je, wajua kuwa kila dakika moja inayopita, kuna seli kati ya alfu 30 hadi 40 zilizokufa zinazodondoka tok katika mwili wa mwanadamu?
5. Je, wajua kuwa ubongo wa mwanadamu umeumbwa kwa maji kwa kiwango cha asilimia 80?
6. Je, wajua kuwa kati ya viumbe wote duniani, ni mwanadamu pekee ambaye anaweza kulala kwa kutumia mgongo wake?
7. Je, wajua kuwa ukubwa wa jicho l mwanadamu daima ni ule ule toka anapozaliwa hadi anapozeeka? Pua n masikio hukua kwa kadiri mwanadamu anavyozidi kukua.
8. Je, wajua kuwa paka ana uwezo w kubadili sauti yake na kufanya milio zaidi ya 100 tofauti tofauti wakati mbwa ana uwezo wa kufanya hivyo na kutoa sauti kumi tu?
9. Je, wajua kuwa visiwa vya Hawaii huvisogelea vile vya Japan kwa umba wa inchi 4 kila mwaka?
10. Je, unajua kuwa kutengeneza karatasi mpya kutokana na karatasi z zamani zilizoisha matumizi yake kunaweza kusaidia kupunguza matumizi ya nishati kwa asilimia takriban 70 kulinganisha na kutengeneza karatasi hizo kutokana n miti
Jifunze Zaidi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment