SAYARI YA MARS!


Mars (Mirihi) ni sayari ya nne katika mpangilio wa Sayari kutoka lilipo Jua katika mfumo wetu wa Jua.
Mars ni sayari ya pili kwa udogo katika Sayari zinazotambulika katika mfumo wa Jua.
Jina la "Mars" linatokana na jina la mmoja miungu wa ki-Rumi (Mars)... Kutokana na tamaduni za ki-Rumi: Mars alikuwa mungu wa Vita aliyeheshimika sana kwa wa-Rumi, namba mbili kwa mungu Jupiter tu.
Mars, huitwa pia, kwa jina: 'Red Planet', kutoka na wekundu wa rangi yake unaotokana na 'iron oxide' ambayo ipo kwa wingi kwenye ardhi yake...
Mars ina sifa kadhaa za kujidai, kwa mfano: Ina mlima mrefu kuliko milima yote kwenye sayari zilizopo mfumo wetu wa jua. Mlima huo unaitwa 'Olympus Mons', na pia ina moja ya ma-crater makubwa katika mfumo wetu wa Jua, crater hilo linaitwa 'Valles Marineris'.
Mars ina miezi miwili, inayoizunguka... Miezi hiyo ni: Phobos na Deimos.
Jitihada zetu kuitafiti Mars:
Utafiti na Uchunguzi wa Sayari hii umeendelea kwa mamia ya miaka sasa, ukianza na ugunduzi wa telescope miaka ya 1600...
Kwa miaka mingi, watu wameiangalia Mars kwa shauku kubwa, wakajaribu ku-imagine mazingira yake, na wengine hata kuhisi, pengine kuna viumbe vingine vyenye akili (intelligent life) kwenye Sayari hiyo...
Kutoka karne ya ishirini, vyombo kadhaa vya anga (probes) vimetumwa ndani ya sayari ya Mars, na vingine karibu na angahewa (atmosphere) yake ili kujaribu kujua zaidi kuhusu Sayari hiyo...
Vyombo hivyo vimetusaidia kuongeza maarifa yetu kuhusu Sayari hiyo, geologia (geology) yake, na hata uwezekano wa kuishi huko...
Kusafirisha vyombo vya utafiti kwenda Mars, si kazi ya kitoto... Ni kazi complicated, ambayo inabidi ku-consider mambo kibao. Na, ndio maana mission nyingi za kutuma vyombo kwenda Mars zimeishia kufeli (zaidi ya 2/3 ya mission kwenda Mars zimefeli mpaka sasa). Vyombo vingine vilifika, lakini vikashindwa kuripoti chochote kutokana na hitilafu mbalimbali...
Lakini, pamoja na ugumu huo, kuna mission kadhaa, zilizofanikiwa, na kuzaa matunda, kama zile rover mbili mapacha zilizopo Mars hivi sasa...
Tangu tarehe 6 Agosti 2012, kuna vyombo (rovers) vilivyopo Mars vinavyoendelea kutuma taarifa kuhusu Mars kuja Duniani. Vyombo hivyo ni 'Opportunity' na 'Curiosity'... Pia kuna vyombo (orbiters) vitatu vinavyozunguka Mars ambavyo ni: 'Mars Odyssey', 'Mars Express' na 'Mars Reconnaisance Orbiter'.
Ifahamike pia kwamba: Mpaka sasa, hakuna sample (mchanga, mawe, maji, n.k) kutoka Mars zilizoletwa Duniani... Kuna mission moja ilitaka kufanya kazi hiyo ya kuchukua sample, na kuzileta duniani; lakini ikashindwa...
Tafiti mbalimbali zilizofanya na vyombo hivyo, vimetupa ushahidi wa kutosha kudai kwamba: "Kuna kipindi kulikuwa na maji (liquid water) katika Mars"... Zimetuwezesha pia kuijua geolojia, pamoja na hali ya hewa kwenye Sayari hiyo... Kuhusu uwepo wa maisha katika Sayari hiyo, bado hakujawa na ushahidi Kuhusu hilo...

No comments:

Post a Comment

Active Visitors

Pages