'Kepler' ni chombo cha uchunguzi cha anga (space observatory) kilichotengenezwa na NASA, kwa dhumuni la kutafuta Sayari nyingine zinazofanana na Dunia, zinazozunguka nyota nyingine...
Kifaa hicho kilirushwa tarehe 7, Machi 2009, na kimepewa jina hilo (Kepler) kumuenzi mwanaAstronomia Johannes Kepler.
Kifaa hicho kimetengenezwa kuchunguza eneo tu la galaksi yetu (Milky Way).
Dhumuni kubwa la chombo kama nilivyosema awali ni: Kutafuta Sayari nyingine zinazofanana na Dunia (Earth-like planets) au zile zilizo umbali sahihi kutoka nyota yake (habitable zone) unaoiwezesha kufanana na Dunia.
Lengo lingine la chombo hiki likiwa ni kujua kuna nyota ngapi katika mabilioni ya nyota kwenye galaksi yetu, zenye sayari kama hizi zinazofanana na Dunia...
Nini maana ya "Kufanana na Dunia"?
Dunia ipo kwenye kundi la Sayari, tunazoziita "Sayari za mwamba" (Rocky Planet/Terrestrial Planet).
Sayari za mwamba zimeundwa kwa kiasi kikubwa na mwamba na madini... Katika mfumo wa Jua, Sayari hizi za mwamba huwa ni zile zilizo karibu na Jua.
Sayari nyingine tofauti ni Sayari kama "Sayari jitu za gesi" (gas giants) ambazo zimeundwa kwa kiasi kikubwa na gesi kama hidrojeni na heli. Mfano mzuri wa Sayari hii ni Mshtarii (Jupiter).
NB: Mpaka kufikia Januari 2013, Kepler imewawezesha wanaSayansi kuorodhesha Sayari takribani 2,740 zinazofanana na Dunia...
Sayari hizo ni kama:
'Kepler-1b', 'Kepler-2b', 'Kepler-3b', 'Kepler-4b', 'Kepler-5b', 'Kepler-6b', 'Kepler-7b', 'Kepler-8b', 'Kepler-9b'...
Na nyingine kibao...
Kituo cha 'Ames Research Center' kilichopo jijini California nchini Marekani ndio kinatumika kuongoza chombo hiki pamoja na ku-analyse data zinazotumwa na chombo hiki.
Kepler ilikuwa imepangwa kudumu kwa muda wa miaka mitatu na nusu tu, lakini muda wake umeongezwa mpaka ifikapo mwaka 2016, na hii ni kutokana na kwamba: data inazotuma ni nyingi mno, na inachukua muda mrefu kuzi-analyse...
So, next time ukiangalia juu, kumbuka kuna chombo kiitwacho 'Kepler' kipo kikipiga kazi...
IJUE 'KEPLER'
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment