NYOTA KONGWE KULIKO ZOTE YAGUNDULIWA!


Nyota ambayo imekuwa ikifahamika kwa muda mrefu sasa, yenye jina "HD 140283" ambayo ipo umbali wa miaka 190 ya nuru kutoka hapa tulipo, imegundulika kuwa ndio nyota kongwe kuliko zote ukilinganisha na nyota zote tunazozifahamu...
Nyota hiyo ina miaka takribani bilioni 13.2...
Kuna uwezekano pia, ikawa kongwe zaidi, kwani tafiti za awali zilionesha ina miaka kama bilioni 13.9, lakini baada ya kujumlisha na uwezekano wa kosa la upimaji (experimental error), ikaja namba hiyo ya miaka bilioni 13.2.
Nyota hii, ni moja ya nyota za kwanza kwanza kabisa kuzaliwa mara baada ya "BIG BANG"... Kwani tunaamini "BIG BANG" ilitokea takribani miaka bilioni 13.7 iliyopita...
Ujasiri zaidi wa kusema nyota hii ni kongwe zaidi, ni kwasababu imeundwa kwa asilimia kubwa mno na hidrojeni pamoja na helium tu, kwani elementi nyingine hazikuwa kwa wingi kipindi hicho...
Nyota nyingine ambayo awali ilikuwa inajulikana kuwa kongwe kuliko zote ni "Methuselah"... Lakini "HD 140283" inaonekana kuwa kongwe zaidi...
MwanaAstronomia aliyetangaza na kufanya utafiti huu pamoja na timu yake anaitwa Howard Bond, anayefanya kazi katika kitengo cha Astronomia katika chuo cha Pennsylvania...
NB: Nyota yetu (Jua) ina miaka takribani bilioni 4.6, na bado ni kijana anayechipukia, ukilinganisha na nyota nyingine...

No comments:

Post a Comment

Active Visitors

Pages