DUNIA YETU!


Tuna kila sababu ya kujivunia Sayari yetu nzuri... Dunia yetu yenye jina "Sayari ya bluu" (Blue Planet), imepewa jina hilo kwani karibu asilimia 70 imezingirwa na maji.
Nadhani si habari ngeni kwamba, Dunia ni sayari ambayo sisi sote twaishi. Na pia, ni sayari pekee ambayo mpaka sasa twafahamu ina uwezo wa kumudu kuwa na "maisha".
Kuna sayari nyingine ambazo wanaSayansi wanahisi zaweza kuwa na maisha, lakini hata hizo pia ni kwasababu zinafanana kwa namna moja ama nyingine na Dunia yetu.
Dunia yetu yaweza kumudu kuwa na maisha kwasababu ipo umbali wa kilomita 147,098,291 kutoka Jua ikiwa karibu, na kilomita 152,098,233 ikiwa mbali. Ipo umbali sahihi kupokea kiasi cha mwanga na mionzi ili kuwa na joto, ambalo maisha yaweza kustahimili...
Angahewa (atmosphere) la Dunia ina mchanganyiko wa Nitrojeni ambayo inachukua asilimia 78.09 (Nitrojeni ni moja ya viungo muhimu katika DNA yetu), vilevile kuna Oksijeni yenye asilimia 20.95 (ambayo bila hiyo tusingeweza pumua)...
Dunia yetu ina mwezi mmoja...
Nadharia iliyopo sasa, inapendekeza kuwa: Hapo awali, mwezi ulikuwa sehemu ya Dunia, mpaka Dunia ilipogongana na gimba (body) lingine, hivyo kufanya sehemu ya Dunia imeguke, na kubaki ikielea angani...
Bado kuna mengi tusiyoyafahamu kuhusu Dunia. Mengi tunayoyafahamu kuhusu namna sayari yetu ilivyo kwa ndani, inatokana na makadirio ya kiSayansi kwa kuangalia yanayotokea kwenye sayari yetu.
Kwa kuchunguza muundo Dunia, twafikiri kiini (core) cha ndani cha Dunia kimeundwa hasa na chuma, pamoja na nikeli.
Kiini cha nje kina hali ya kiowevu kutokana na joto kali. Mnato wake huuaminiwa kufanana na maji, halijoto yake ni kati ya 4,000 - 5,000 °C.
Kiini cha ndani ni sehemu yenye joto kushinda yote duniani. Kiwango cha halijoto kinapita 5,000 °C. Lakini chuma kinaaminiwa kuwa imara si kiowevu kwa sababu ya shindikizo kubwa.
Kila ukikaa, na kuangalia nyota na kuwaza: "Kuna nini huko nje?", Kumbuka: "Tunaishi kwenye Dunia ya ajabu, nzuri na ya kupendeza, yenye maswali mengi pia, ambayo yanasubiri kujibiwa..."

No comments:

Post a Comment

Active Visitors

Pages