Je! Ulimwengu huu tunaouona, upo peke yake?
Je! Kuna uwezekano wa kuwa na Ulimwengu mwingine ambao hatujautambua bado?
Vipi kama kuna Ulimwengu zaidi ya mmoja au miwili... Vipi kama kuna maelfu ya Ulimwengu???
Inaonekana kama Hadithi fulani ya kufikirika au muvi ya sci-fi ya Hollywood eeh?
Well, Nikufahamishe kwamba: Kuna WanaSayansi wanaochukua idea hiyo very seriously.
Hii Ni Nadharia ya "Multiverse" (Ulimwengu zaidi ya mmoja), au kama wenzangu na mimi ambao ni wapenzi wa "Science Fiction", tunaifahamu kama: "PARALLEL UNIVERSES".
Idea hii ya WanaSayansi hawa inatokana Nadharia moja iitwayo "Eternal Inflation", ambayo inasema muda mfupi baada ya "BIG BANG" kutokea ambayo ndio iliyosababisha kuzaliwa kwa Ulimwengu huu tunaouona, anga na wakati (space-time) vilipanuka tofauti kati ya sehemu na sehemu... Na hii ikasababisha vi-Ulimwengu vingine kuzaliwa.
Kila Ulimwengu uliozaliwa una sheria tofauti za fizikia (laws of physics)...
Nadharia hii ya Ulimwengu zaidi ya mmoja imekuwa kama hadithi tu kwa muda mrefu, lakini sasa kuna wachunguzi waliodai kwamba: Kama kuna Ulimwengu zaidi ya mmoja, itakuwa kuna kipindi Ulimwengu na Ulimwengu mwingine hugongana, na kama hilo likitokea; basi lazima kutakuwa na mionzi fulani inayotengezwa kutokana na mgongano huo (CMB radiation)... na kama basi mionzi hiyo ikipatikana; inaweza ikatufanya tufikiri mara mbili kuhusu hilo...
Pamoja na hayo; Bado kwa wengi, idea kwamba kuna Ulimwengu zaidi ya mmoja, inabadilisha kila kitu kuhusu mtazamo wao juu ya mambo mengi na maisha kwa ujumla wake...
Lakini kwa Upande mwingine pia inatufanya kuelewa baadhi ya tabia na kujibu baadhi ya maswali kuhusu Ulimwengu tunaouona...
Kwa mfano: Kwanini Ulimwengu wetu una viumbe hai (maisha)? Kuna muda ukiangalia baadhi ya konstanti na sheria zake za kiFizikia ni kama vile ziliwekwa na mtu... Maana kama graviti isingekuwa ilivyo pamoja na konstanti nyingine, basi maisha yasingekuwepo.
Lakini tukitumia Nadharia ya Ulimwengu zaidi ya mmoja, na kwamba kila Ulimwengu una sheria tofauti za Fizikia, basi kuna Ulimwengu mwingine hauna maisha, na Ulimwengu mwingine unao, na yote hayo ni kwasababu ya bahati (coincidence)...
Bado vile vile, zamani sana watu waliamini Kuna sayari moja tu ambayo ni Dunia, na inazungukwa na Jua na Nyota sababu hawakuwa na vifaa vya kuona mbali zaidi ya macho yao... Lakini vifaa na maarifa yalivyoongezeka, wakajua kuna sayari zaidi ya moja.
Lakini bado tena wakaamini kwamba kuna mfumo mmoja tu wa Jua (solar system) ambao ni wetu... lakini maarifa yalivyoongezeka wakagundua kuna mamilioni ya mifumo hii katika galaksi...
Lakini bado tena wakadhani kuna galaksi moja, na muda si mrefu katika karne ya ishirini tu, tumegundua kuna mabilioni ya galaksi katika Ulimwengu...
Sasa tunaamini kuna Ulimwengu mmoja, kwasababu vifaa tulivyonavyo havituwezeshi hata kuona mwisho wa Ulimwengu huu...
Swali linakuja: Vipi kama Historia ikijirudia tena, na tukagundua kuna Ulimwengu zaidi ya huu tunaouona...?
Nadharia hii imetokea kufurahisha akili za watu wengi kama mimi tunaopenda ku-Imagine maisha na Ulimwengu mwingine zaidi ya huu...
Kuna WanaSayansi wengine wameenda mbali na hata kudai kwamba, Hata mtu mmoja kama wewe, yaweza kuwa upo kwenye Ulimwengu mwingine... Pengine huyo mtu kama wewe kwenye Ulimwengu mwingine, ana tabia tofauti kidogo na wewe...
Idea hii mara nyingi yanifanya niwaze: Kama kuna "John" mwingine kama mimi katika Ulimwengu mwingine, yukoje? Je! anapenda Sayansi kama mimi? Je! Anapenda vitabu kama mimi? Na Je! ni mbishi kama mimi? hahaha....
Nadharia hii ya Ulimwengu zaidi ya mmoja ni pana, na si rahisi tu kama nilivyoeleza. WanaSayansi wengi wanakubali uwezekano kwamba yaweza kuwa na Ulimwengu zaidi ya mmoja. Lakini Naomba ifahamike kwamba: Mpaka sasa Hakuna Ushahidi wa kutosha kwamba kuna Ulimwengu zaidi ya huu tunaouona...
Mmoja ya WanaSayansi ambaye amekuwa akiibebebea bango nadharia hii kwa muda mrefu sasa na ambaye ni mmoja ya wanaSayansi naowakubali mno, anaitwa Brian Greene; na ameandika kitabu kizuri kinachoelezea vizuri nadharia hii na zaidi... Kitabu hicho kinaitwa "HIDDEN REALITY"!
NADHARIA YA ULIMWENGU ZAIDI YA MMOJA (MULTIVERSE)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment