MASWALI AMBAYO BADO HAYAJAJIBIWA NA SAYANSI:


Sayansi ni ya muhimu katika jamii, na katika karne kadhaa zilizopita; Sayansi imeweza kutupatia majibu kadha wa kadha iwe ni Tafiti za Sayari na Anga, dawa kwa maradhi na kutuwezesha kuifahamu Dunia yetu ambayo twaishi...
Pamoja na hayo yote, bado kuna mambo mengi ambayo Sayansi haina majibu, mfano mzuri tu ni kwamba: wanaAstronomia wanakiri mpaka sasa tunfahamu tu asilimia nne (4%) ya Anga, nayo pia ni anga tunayoweza kuiona (observable Universe), bado kuna asilimia kama 96 inasubiri kugundulika...
Kumekuwa na fikra miongoni mwa watu wengi kwamba wanaSayansi ni watu wanaojifanya kujua kila kitu... Sijui fikra hii inatoka wapi, kwani mwanaSayansi ni mtu wa kwanza ku-admit kuwa hajui kila kitu... Na ni shauku hii ya kutaka kujua inayowaendesha wanaSayansi kuendelea kutafiti...
Anyways, nisiongee sana mahali hapo, maana mara nyingi nikianza kuongelea hilo huwa napitiwa... hahaha.
Yafuatayo ni baadhi ya maswali kwa kufikiri tu haraka ambayo ninaona hayajajibiwa, au hayajapata majibu yakuridhisha:
1. Nini kilisababisha "BIG BANG" na hatimaye Ulimwengu kuzaliwa?
- Kuhusiana na swali la Ulimwengu ulianzaje, WanaSayansi wengi wanakubaliana na Nadharia inayoamabatana na ushahidi wa kutosha kwamba, Ulimwengu ulizaliwa baada ya BIG BANG miaka bilioni 13.77 iliyopita.
Lakini Swali lililopo sasa, ni: Nini kilitokea kabla, au nini kilisababisha "BIG BANG"?
Nina uhakika mwanaSayansi kama Lawrence Krauss akinisikia anaweza hata kunipiga kwenzi, Kwasababu, yeye anadai: "Kabla ya BIG BANG hakukuwa na anga (space) wala wakati (time), kwahiyo kuuliza swali kama: Nini kilitokea kabla ya BIG BANG haina maana yoyote, kwasababu hakukuwa na chochote (nothing)." Na Lawrence ameandika kitabu kizima kuelezea namna kila kitu kinaweza kutokana na hali ya kutokuwa na kitu (nothing)...
Ni kweli kwamba ukiangalia maelezo pamoja na Hesabu zake waweza kushawishika, Lakini fact ni kwamba: Hayo ni mawazo yake ambayo bado hayajakubalika kwa pamoja na wanaSayansi wote kwahiyo, swali bado lipo pale pale.
2. Nini Maana ya Ufahamu (Consciousness)?
- Kwa haraka haraka laweza kuonekana kama swali rahisi mno, Na ninadhani hata nikimuuliza mtu: Nini maana ya Ufahamu? anaweza akanipa jibu baada ya sekunde kadhaa...
Lakini ukweli ni kwamba: Mpaka sasa, bado Sayansi haijatoa jibu lenye Uhakika kuhusiana na Ufahamu (Consciousness).
Kuna Nadharia kadha wa kadha sasa kuhusu maana na chimbuko la Ufahamu... WanaSayansi wengine wameenda hata mbali na kudai, field ya "Quantum Mechanics" inaweza kuhusika katika Ufahamu.
Wengine wetu, ikiwemo mimi, tunaamini kwamba jibu la: Nini maana ya Ufahamu, litakuja kadiri tunavyozidi kuboresha teknolojia za kutengeneza roboti na mashine nyingine zinazofikiri (Artificial Intelligence).
3. Kuna Sayari ngapi katika Mfumo wetu wa Jua(Solar System)?
- Laweza kuonekana kama swali la ajabu, Lakini tangu Pluto iliposhushwa kutoka ligi daraja la Sayari na kwenda ligi ndogo ya "Sayari Kibete" (dwarf planet); hatuna uhakika kama hizo Sayari nane zilizobaki pamoja na Jua ndo kila kitu.
Inaonekana ajabu eeh? Kwamba twaweza kujua kuhusu nyota iliyo miaka ya nuru kadhaa, lakini hatujui kuna nini nyuma ya mlango wetu tu...
Ukweli ni kwamba: Sehemu kubwa ya Mfumo wetu wa Jua, bado hatuijui na haijakanyagwa...
Eneo kati ya Utaridi (Mercury) na Jua lina mwanga mno, kiasi kwamba hatuwezi kuona chochote. Na eneo nyuma ya Uranus lina giza mno na hatuwezi kuona. WanaSayansi bado wanagundua magimba mapya katika ukanda wa Asteroidi karibu kila siku...
Na kuna baadhi ya wanaAstronomia wanaoamini kuna jua la pili katika mfumo wetu wa Jua. Seriously???
4. Kuna spishi (species) aina ngapi za wanyama waishiyo Duniani?
- Katika karne hii ya 21, siku za Marco Polo na wagunduzi wa maeneo mapya katika Dunia zimeshapita. Yaani tayari tuna ufahamu wa maeneo yote Duniani. Unaweza ukadhani kwamba kwa ufahamu, basi twaweza toa idadi ya aina ngapi za spishi za wanyama tulio nao Duniani, ambao bado hatujawaua ukizingatia ukatili wetu kwa wanyama.
Ukweli ni kwamba hatupo hata karibu kujua tuna spishi ngapi... Kila mwaka tunagundua karibu spishi 15,000 mpya.
Mpaka sasa tumeshakusanya rekodi ya spishi kama milioni mbili hivi... Na wanaSayansi wanakadiria kwamba jumla ya spishi za viumbe viishivyo duniani ni kama milioni 5 mpaka milioni 100.
5. Kwanini Barafu Inateleza?
- Kusema kwamba: Barafu huteleza ni sawa na kusema Maji yamelowa...
Ni jambo tulilofahamu kwa muda mrefu kwamba barafu huteleza, jambo ambalo hatujajua ni: Kwanini Barafu huteleza?
Soo funny!
Je! Una mifano wa maswali mengine ambayo unahisi bado hayajajibiwa? Tuambie!

No comments:

Post a Comment

Active Visitors

Pages