Mkono wa kwanza wa kibioniki (bionic hand) unaomuwezesha aliyewekewa kuweza kuhisi vitu anavyovigusa kama mkono wa kawaida vile umeweza kutengenezwa
Mtu mwenye bahati ya kuwa wa kwanza kuutumia mkono huo ni kijana wa miaka 20 aishiye Roma, Italia; ambaye alipoteza sehemu ya mkono wake kufuatia ajali mbaya aliyopata.
Dr. Micera, ambaye ni mmoja ya wanaSayansi watakaohusika kuupachika mkono huo, amesema: "Mkono huu utaunganishwa kwenye mfumo wa hisi (nervous system) kwa kuunganisha elektrodi zake kwenye "vipokea hisia" (nerves) vya mkono". Hii itamwezesha aliyewekewa mkono huo kuweza kuu-control mkono huo, na hata kupokea hisia za kuguswa.
Kwasababu, mkono umeunganishwa kwenye mfumo wa Hisi (nervous system), ina maanisha: aliyewekewa ataweza kuu-control mkono huo kwa kutumia Ubongo, kama wafanyavyo watu wenye mikono ya kawaida. Mkono huo utakuwa ukipokea na kutuma taarifa kwenye Ubongo kupitia mfumo huo wa hisi.
Dr. Micera aliendelea kusema: "Hii inakuja kama taarifa njema, kwa wale ambao kwa namna moja ama nyingine wamepoteza mikono yao..." Na hii ni hatua kubwa katika Ulimwengu wa Sayansi...
MKONO WA KWANZA WA KI-BIONIKI (Bionic hand) WENYE UWEZO WA KUHISI...
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment