"Cloud Seeding" ni aina ya ujuzi inayotumika kupandikiza mvua na hata theluji (snow) katika mawingu.
Hii huwezekana kwa kupandikiza chembe katika mawingu zenye maji yaliyogandishwa mno (supercooled water).
Upandikizi huu waweza kufanyika kwa genereta maalum kwenye ardhi, au kwa kutumia ndege au rocket.
Mvua hutokea pale ambapo chembe hizo huchangamana na chembe nyingine za vumbi, chumvi au mchanga na kutengeneza 'crystal' za barafu. crystal hizi hutengeneza nucleus na matone ya maji huanza kutengenezeka. Baada ya muda matone haya huongezeka uzito na kuanguka kama mvua.
Dhana hii ya "Cloud Seeding" ilianza mwaka 1946, wakati mwanaSayansi Dr.Vincent Schaefer akifanya utafiti wa namna ya kutengeneza mawingu katika chumba maalum. Schaefer aliongeza barafu katika jaribio moja ili kuongeza ubaridi katika chumba; kwa kufanya hivyo akagundua kwamba matone ya maji yalianza kutengenezeka katika mawingu...
Kutoka hapo, "Cloud Seeding" imekuwa ni technique inayotumiwa na nchi mbalimbali ili kutengeneza na hata kuzuia mvua.
Mfano: mwaka 2008, Beijing waliitumia technique hiyo kuzuia mvua kwa ajili ya michezo ya Olimpiki. Na pia, Marekani hutumia technique hiyo kwa ajili ya kuongeza mvua katika maeneo yanayoonekana kuwa na ukame.
Nchi kama Mali na Niger barani Afrika hutumia pia technique hii kama namana ya kuongeza mvua...
Waweza kujua zaidi kuhusu "Cloud Seeding" kwa kutembelea page hii katika wikipedia:
http://en.wikipedia.org/wiki/
Cloud_seeding
(HomeWork: Kama upo fiti, nisaidie kunipa msamiati wa Kiswahili wa "Cloud Seeding")
CLOUD SEEDING!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment