LADY GAGA NA WASANII WENGINE KWENDA SAFARI YA ANGA!


Msanii maarufu wa Ki-Marekani, Lady Gaga anatarajia kusafiri safari ya Anga kwa kutumia Chombo cha 'SpaceShipTwo' cha shirika la 'Virgin Galactic' kitakachoanza safari zake mwisho wa mwaka huu, au mwanzoni mwa mwaka ujao.
Gaga, pamoja ma-super star wengine kama Justin Bieber, Leonardo DiCaprio pamoja na Ashton Kutcher, tayari wameshakata tiketi zao kwa ajili ya safari hiyo.
Tiketi moja katika Chombo hicho inagharimu kiasi cha dola za ki-Marekani 250,000. Ambayo ni sawa na takribani milioni 400 za ki-Tanzania. Tayari watu 600 wameshakata tiketi kwa ajili ya safari kutumia chombo hicho.
Chombo hicho cha 'SpaceShipTwo' ambacho kimetengenezwa maalumu kwa ajili ya Utalii wa Anga (Space Tourism) kitakuwa kikifanya safari zake kutoka angahewa la Dunia, na kisha kurudi tena Duniani...
(So, kama vipi tuanze kujibana na sisi tupate nafasi ya kukata tiketi kwenye chombo hicho... au sio? hahaha)

No comments:

Post a Comment

Active Visitors

Pages