INDIA NAO HAWAPO NYUMA; WATUMA CHOMBO CHAO CHA ANGA KWENDA MARS


Ilikuwa ni Jumapili ya Desemba 1 ambapo India wametuma chombo chao cha kwanza kabisa cha Anga kwenda Sayari ya Mirihi ijulikanayo kwa jina maarufu la Kingereza kama Mars.
Chombo hicho kinatarajiwa kufika kwenye obiti (orbit) ya Mars ifikapo Septemba ya mwaka Kesho. Mafanikio ya chombo hichi yataifanya India kuingia katika klabu ya nchi chache zilizofanikiwa kutuma vyombo vyao kwenye obiti na hata kutua kwenye Sayari hii ya Mars.
Nchi hizo ni kama Marekani na Urusi.
Chombo hichi cha India, kiitwacho 'Mangalyaan' kitakutana na changamoto nyingi sana njiani, kwani zaidi ya nusu ya vyombo vinavyotumwa Mars hukutana na misukosuko na kushindwa kufika.
Chombo hicho kilichoigharimu India dola za Ki-Marekani takribani Milioni 72, kinatarajiwa kufanya tafiti mbalimbali, ikiwemo kutafuta gesi ya Methane katika angahewa ya Mars.
Sasa, Utafiti wa anga umeshaanza kuleta Ushindani mkubwa kati ya nchi, Ikiwemo China ambayo jana tu imetuma chombo kwenda Mwezini, na bado ikiwa na ndoto pia ya kumtuma mtu wao kukanyaga Mwezi ifikapo 2020. Hii yote ni Habari njema sana kwa Ulimwengu wa Sayansi.
Hii ni hatua kubwa sana iliyochukuliwa na India, na kwa hakika wanastahili Pongezi...

No comments:

Post a Comment

Active Visitors

Pages