Kutana na "ATHLETE", chombo kingine cha NASA kwenda mwezini...
Ni mpango wa NASA kujenga na kuwa na makao kwenye mwezi, lakini ili kujenga makao hayo na kufanya shughuli nyingine ndogo-ndogo, wanaAnga wa NASA watahitaji vyombo vya usafirishaji...
Lakini kuna shida moja: Hakuna barabara mwezini! Na ndio maana, mainjinia wa NASA, wame-design chombo kiitwacho "ATHLETE" ili kumudu mazingira yoyote, iwe ni yenye vumbi, mawe na hata mabonde...
ATHLETE (All-Terrain Hex-Limbed Extra-Terrestrial Explorer).
Chombo hicho kina miguu sita kama buibui inayojipinda pamoja na matairi chini. Kwenye mazingira laini: inatembea kwa matairi yake, ikikutana na kikwazo mbele mfano, jiwe: inalipanda na kulivuka.
ATHLETE vilevile inaweza kujigawa kuwa roboti kadhaa, na inaweza kujiunga tena...
Sehemu za ATHLETE kwa namba:
1. ATHLETE ina camera 48, zinazorekodi na kutoa video kwa teknolojia ya 3-D... Inaishinda chombo kingine cha "CURIOSITY" chenye camera 17...
2. Chombo kinaweza kujaza tena seli zake zenye mafuta ya hidrojeni kwenye vituo vya angani, vinavyotumia nguvu ya jua (solar) vinavyochukua maji, na kuyagawanyisha kuwa hidrojeni, pamoja na oksijeni...
3. Miguu yenye matairi ya ATHLETE yanaiwezesha kutembea, na kupanda kutegemeana na mazingira.
4. Vifaa vya kuchimba na kubeba sample za mawe na mchanga kwa ajili ya utafiti.
5. Klampu kwenye matairi huweza hubeba vifaa mbalimbali...
6. Mkanda ambao hubeba na kuhifadhi vifaa ambavyo havitumiki kwa muda huo...
7. Matairi yasiyo na hewa (hayawezi ku-burst au kupata flat)
8. Moja ya roboti zinazoiunda ATHLETE, ambayo kazi yake ni kupokea mizigo inayotumwa mwezini kutoka Duniani...
9. ATHLETE ikiwa imejigawa kuwa vyombo viwili vinavyofanana, vyenye miguu mitatu vinavyoitwa "Tri-ATHLETEs"...
10. ATHLETE inaweza kuinyoosha miguu yake hata kufikia urefu wa futi 27...
11. ATHLETE huweza kutembea katika mazingira yoyote ikiwa imebeba mzigo, na kuuweka "level" ili usianguke...
12. Inapotua mzigo, ATHLETE huishusha miguu yake kwa kuiingiza ndani, mpaka mzigo utue chini salama...
Ijue "ATHLETE",
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment