Uchimbaji wa Asteroidi (Asteroid Mining) washamiri...
Kadiri rasilimali zinavyozidi kupungua Duniani, na idadi ya watu kuongezeka, imewafanya watafiti na wadau mbalimbali kuanza kufikiria njia mbadala...
Kampuni mpya, yenye jina "Deep Space Industries" iliyo nchini Marekani imetangaza mpango wake wa kuzindua vyombo kadhaa vya angani, vyenye uwezo wa kusafiri mpaka ukanda wa Asteroidi ili kufanya uchimbaji...
Asteroidi ni gimba la angani linalozunguka jua kama sayari. Ni ndogo kuliko sayari lakini kubwa kushinda kimondo.
Katika mfumo wetu wa jua kuna angalau asteroidi 338,000 zinazotambuliwa na wanaAstronomia, nyingi zinazunguka katika ukanda wa Asteroidi kati ya njia za Mirii (Mars) na Mshtarii (Jupiter)...
WanaSayansi wamejua kwa muda sasa kwamba kuna utele wa maji pamoja na madini mengine ya thamani katika Asteroidi zilizo karibu na Dunia.
Lakini sasa, kwa mara ya kwanza, makampuni yameanza kuwa serious kutafuta namna ya kuzipata rasilimali hizo...
Vyombo hivyo vya anga vinavyotengezwa na "Deep Space Industries " vimepewa jina "Firefly" ili kuenzi tamthilia moja ya televisheni ya mwaka 2002-2003, niliyokuwa nikiipenda, na bado naipenda mpaka leo, yenye jina "Firefly"
Deep Space Industries~USA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment