Ijue TITAN


Titan ni moja kati ya miezi ya Zohali (Saturn).
Titan ni mwezi mkubwa ukilinganisha na miezi yote ya Zohali, na wa pili kwa ukubwa ukilinganisha na miezi yote iliyopo katika mfumo wetu wa Jua.
NB: Mwezi mkubwa kuliko yote katika mfumo wetu wa Jua unaitwa "Ganymede", na ni mwezi wa Jupiter.
Titan huzunguka sayari ya Saturn kwa siku 15 na masaa 22 (mzunguko mmoja).
Kinachonifurahisha kuhusu Titan, ni kwamba: Ni mwezi pekee katika mfumo wetu wa Jua ambao una angahewa (atmosphere).
Na vilevile pia, ni mahali pekee katika mfumo wetu wa jua ukiacha Dunia yetu ambako kuna maeneo makubwa yenye maji au aina fulani ya kimiminika...
Mwezi huu wa Titan uligunduliwa mwaka 1655 na mwanaAstronomia wa ki-Holanzi anayeitwa Christiaan Huygens, na ulikuwa mwezi wa tano, ukiacha mwezi wetu kugunduliwa.
Angahewa ya Titan imeundwa kwa asilimia kubwa na gesi ya Nitrojeni, na ina mawingu ya "Methane" na "Ethane".
Titan vile vile ina hali za hewa kama upepo, na hata mvua, na ina mandhari fulani zinazofanana na Dunia, kama maziwa, bahari na hata mito.
Bahari na mito hii inaonekana kuwa ya kimiminika cha Methane (Liquid Methane).
Titan huwa na joto linalocheza kwenye nyuzi joto -179 °C (Ni mahali penye baridi mno).
Kingine kinachonifanya niione Titan kama sehemu inayonivutia ni kwamba: WanaSayansi wanahisi kwa kiasi kikubwa kwamba kuna aina fulani ya maisha katika mwezi huu wa ajabu.

No comments:

Post a Comment

Active Visitors

Pages