HISTORI YA DINOSAURI (DINOSAURS)


Dinosauri ni kundi kubwa la wanyama walio katika kundi la "clade Dinosauria".
Dinosauri waliishi katika kipindi tunachokiita "Triassic" (kadiri miaka milioni 230 iliyopita).
Dinosauri lilikuwa kundi la wanyama walioshamiri sana katika kipindi hicho cha miaka.
Dinosauri walipukutishwa na kuwa Historia kwenye kipindi cha "Cretaceous" (kadiri miaka milioni 66 iliyopita)
Kumekuwa na Nadharia kadhaa, juu ya nini kilichotokea kusababisha hali hiyo. Lakini, wanaSayansi wengi, wanaamini katika kipindi hicho Dunia iligongwa na Asteroidi, kusababisha mlipuko mkubwa; hali iliyofanya karibu asilimia 75 ya viumbe kuteketea kabisa, Dinosauri wakiwa miongoni mwao.
Ushahidi wa tukio hilo upo kule Mexico, kwenye bonde la "Chicxulub crater" lenye upana wa kilomita 180, na ndipo wanaSayansi wanadhani Asteroidi hiyo ilitua...
Waweza kujiuliza, wanaSayansi wamejuaje wanyama hao walikuwepo duniani. Jibu ni rahisi, nalo ni: VISUKUU (fossils).
Visukuu ni mabaki ya viumbehai ama mimea au wanyama kutoka zamani (miaka 10,000 au zaidi). Visukuu vingi vina miaka mamilioni.
Kwa kusoma visukuu hivyo, wanaSayansi wamegundua kulikuwa spishi kibao za Dinosauri (zaidi ya spishi 700 zimeshagundulika).
Dinosauri wengine walikuwa wala nyasi (herbivorous), na wengine nyama (carnivorous). Kulikuwa na waliotembea ardhini, na wengine walikuwa ndege.
Dinosauri wengi walikuwa ni wanyama wakubwa. kwa mfano, spishi inayoitwa "sauropods" walikuwa na urefu kwenda mbele wa hadi mita 58 (futi 190), na urefu kwenda juu wa hadi mita 9.25 (futi 30 na inchi 4)
Dinosauri wote walipata watoto kwa njia ya kutaga mayai kama reptilia na ndege wafanyavyo sasa.
Tangu kisukuu cha kwanza cha Dinosauri kilipogundulika katika karne ya 19, Visukuu vya Dinosauri vimekuwa vivutio vikubwa sana katika majumba mengi ya maonesho ya Historia.
Na vitabu pamoja na filamu mbalimbali za Dinosauri kama "Jurassic Park" vimewafanya Dinosauri kuwa sehemu ya tamaduni yetu...
Though, huwa kuna kipindi najiuliza: Hivi kutoweka kwa Dinosauri ni jambo jema kwetu, au hata kama wangekuwepo; tungeweza kuishi nao?

No comments:

Post a Comment

Active Visitors

Pages