IJUE "VOYAGER 1"


"Voyager 1" ni chombo cha anga chenye uzito wa kilogramu 722, kilichorushwa na shirika la NASA tarehe 5, Septemba mwaka 1977, kikiwa na dhumuni la kusoma na kutafiti mfumo wetu wa jua (solar system), na hata kwenda mbele zaidi.
Mpaka sasa kinaendelea kusafiri (yaani kimeshasafiri kwa miaka 35). Na kimeshaenda mbali sana (Hakuna chombo kingine kilichoenda mbali kutafiti anga kama chombo hiki).
Hebu fikiri: Umbali wa kutoka duniani mpaka kwenye jua, ni 1 AU (Astronomical Unit), lakini chombo hiki kimeshasafiri umbali wa 123 AU.
"Voyager 1" kwa sasa ipo kwenye ukanda wa mwisho kabisa wa "heliosphere" (Heliosphere ni sehemu ya anga ambalo linamilikiwa na Jua letu). Kwahiyo, waweza kusema "Voyager 1" inakaribia kutoka kabisa kutoka kwenye mfumo wetu wa jua (Solar System).
Santuri:
Katika "Voyager 1" kuna disc ya Santuri iliyowekwa picha mbalimbali za Dunia na viumbe vyake, salamu za lugha mbambali, nyimbo kadhaa pamoja na taarifa kadhaa za Kisayansi, pamoja na taarifa za mahali Dunia ilipo katika anga...
Nia ya kuiweka disc hiyo ni: Kama kuna viumbe vingine vyenye akili (intelligent life) huko nje, mbali na Duniani, basi tuweze kuwasiliana navyo...
Umeme:
Unaweza ukajiuliza: Ni umeme gani unaosafirisha chombo hiki kwa miaka yote hiyo... Well, Chombo hiki kinapata nguvu yake kutoka madini aina ya "plutonium"... Nguvu yake inatarajia kuisha mwaka 2025...
Mfumo wa Mawasiliano:
"Voyager 1"" iliundwa kuweza kuwasiliana na Dunia hata ikiwa nje ya Solar System. Na inawasiliana muda wote na vituo vitatu vya "Deep Space Network" vilivyopo Duniani.
Kukitokea na hitilafu katika mawasiliano; "Voyager 1" ina uwezo wa kutunza kumbukumbu za mpaka kilobyte 62,500...
Mafanikio:
"Voyager 1" ni chombo ambacho kwa kweli kimetusaidia sana kutupa taarifa zaidi kuhusu mfumo wetu wa Jua (Solar System). Imetupatia pia picha nzuri na taarifa nyingi kuhusu sayari ya Jupiter na Saturn...
Kwa taarifa hizo, tumeweza kujua kwamba kuna Bahari katika mwezi wa Jupiter uitwao "Europa", tumeweza kujua pia kwamba kuna tabia za ki-Volkaniki (volcanic activity) katika mwezi wa "Lo" pamoja na taarifa nyingine nyingi...
Ni wakati ninapoangalia vyombo kama "Voyager 1" ninastaajabu kwa namna, vitu watu wanaweza ku-accomplish... "Voyager 1" ilitengenezwa miaka ya sabini, lakini bado yaendelea kudumu mpaka leo... Natoa Salute yangu kwa wanaSayansi wote wa NASA, Na ninaendelea kuitakia Heri "Voyager 1" katika Safari yake kuelekea mahali ambapo mwingine hajakanyaga!

No comments:

Post a Comment

Active Visitors

Pages