Krakatoa ni kisiwa kinachopatikana
Krakatoa hua inakumbwa na milipuko ya volcano kwa miaka kadhaa, lakini janga kubwa kuwahi kutokea lilikuwa ni lile la mwaka 1883, wakati huo Indonesia ilijulikana kama kama Dutch East Indies.
Mlipuko wa volkano wa Krakatoa mwaka 1883, unajumuishwa kama ni moja ya milipuko iliyo uwa maelfu ya watu katika historia ya milipuko ya volkano.
Volkano ya Krakatoa ili anza kulipuka siku ya jumapili , tarehe 26/8/1883 mchana, na kudumu mpaka Siku ya Jumatatu , tarehe 27/8/1883, asubuhi.
Mlipuko wa volkano huo uliambatana na Tsunami na kusababisha uharibifu kwa zaidi ya 70% ambapo zaidi ya watu 36,417 walipoteza maisha.Madhara yake yalijionyesha sehemu mbali mbali za dunia.
Mlipuko ulikuwa mkubwa ulio sababisha wingu nzito lililoenea kwa takribani zaidi ya km 4,830 ambalo lili toa gesi ya Sulfur kwa zaidi ya tani milioni 20, hii ilipelekea upungufu wa kiwango cha nyuzi joto kwa 1.2C° na kupelekea kipindi cha baridi kilicho dumu kwa miaka 5 Duniani kwote.
Wingu nzito baada ya mlipuko wa tatu lili panda juu na kufikia umbali/
Mlipuko wa tatu ndio mlipuko ulio toa sauti kubwa zaidi kuwahi kusikika katika historia ya Dunia zaidi ya dB 310 ambayo ilisikika zaidi ya umbali wa Km 5,000.
Majivu na uji uji wa moto iliruka kwa zaidi ya km 80 na kuambatana na Tsunami lenye kina cha zaidi ya futi 30 lililo sambaa kwa zaidi ya Km 16.
Inasemekana kabla ya mlipuko kulikuwa na dalili za nyufa na matetemeko ya ardhi lakini watu hawaku chukua tahadhari mapema.
Ukitaka kujua zaidi kuna movies inaitwa " Krakatoa imeeleza matukio yote katika janga hilo".
⭐⭐⭐⭐⭐⭐

No comments:
Post a Comment